Pata taarifa kuu
MAREKANI

Donald Trump kutangaza bajeti kubwa zaidi iliyolenga masuala ya ulinzi na usalama

Wakati rais wa Marekani Donald Trump akitarajiwa kulihutubia bunge la Congress Jumanne ya wiki hii ambapo anatarajiwa kutoa tathmini ya namna bajeti yake itakavyokuwa, ametangaza kuwa ataongeza bajeti ya masuala ya ulinzi kwa asilimia 10 akiongeza matumizi makubwa ya ulinzi na kupunguza misaada ya nje.

Rais wa Marekani, Donald Trump, picha ya tarehe 23 Februari 2017.
Rais wa Marekani, Donald Trump, picha ya tarehe 23 Februari 2017. ©REUTERS/Jonathan Ernst/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Akiwa katika mkakati wa kutimiza ahadi zake alizozitoa wakati wa kampeni za urais, rais Trump amejikita katika kuhakikisha anatekeleza ahadi yake ya usalama kwa raia na usalama wa taifa.

Viongozi wa ikulu ya Washington wanasema kuwa, Trump amepanga kuweka nyongeza ya dola bilioni 54 katika masuala ya ulinzi na kupunguza matumizi mengine ambayo hayahusiani na masuala ya kijeshi.

Hatua yake hii itashuhudia kupunguzwa kwa kiasi kikubwa bajeti za baadhi ya maeneo na maeneo mengine kuwekwa masharti makali ili kukusanya fedha ambazo zitaelekezwa katika majeti yake ya ulinzi.

Rais Trump ameahidi kujenga ukuta kwenye mpaka wa nchi yake na Mexico, kufukuza wahamiaji haramu na kuwatokomeza wanajihadi kwenye uso wa dunia.

Bajeti yake itahitaji idhini ya bunge la Congress, suala ambalo wachambuzi wa mambo wanaona kuwa itapitishwa kutoka na chama chake cha Republican kuwa na umiliki katika mabunge yote.

Hatua yake hii itaongeza maradufu bajeti ya nchi hiyo kwenye masuala ya ulinzi, bajeti ambayo hata kwa sasa ni kubwa zaidi kuliko nchi nyingine yoyote duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.