Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-SERA ZA NJE

Donald Trump asaini agizo jipya kuhusu wahamiaji

Baada ya ghasia zilizosababisha agizo la kwanza kuhusu wahamiaji la rais wa Marekani, kusimamishwa na mahakama, Ikulu ya White House imetangaza kwamba agizo jipya limesainiwa. Agizo hilo linatarajiwa kuwa lenye mafanikio zaidi, Ikulu ya White House imebaini.

Rais Donald Trump amesaini agizo jipya kuhusu Uhamiaji, Machi 6, 2017.
Rais Donald Trump amesaini agizo jipya kuhusu Uhamiaji, Machi 6, 2017. REUTERS/Carlos Barria/FILE
Matangazo ya kibiashara

Kama kwenye agizo la awali raia kutoka nchi saba walilengwa, Hatimaye nchi sita zinalengwa kwenye agizo hili jipya. Iraq imeondolewa kwenye orodha na watu waliopewa visa au hati nyingine za serikali sasa watalindwa.

Kukosekana kwa Iraq kwenye orodha hii ni mabadiliko ya kwanza makubwa kwenye rasimu hii ya agizo jipya kuhusu wahamiaji. Hoja za wabunge, askari waliopigana nchini Iraq, na serikali ya Baghdad, ndizo zilishawishi Ikulu y White House kubadili msimamo, mwandishi wetu katika Washington, Anne-Marie Capomaccio, amearifu.

Ni vigumu kupiga marufuku kuingia nchini Marekani, askari au wakalimani kutoka Iraq ambao waliendesha kazi yao sambamba na askari wa Marekani. Wizara ya mambo ya Nje ya Iraq pia imeelezea "kuridhika" kwake na uamuzi huu. Rex Tillerson, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, ameelezea kwa kina sababu zilizopelekea serikali ya Marekani kuiondoka Iraq, mshirika wake muhimu, kwenye orodha hiyo.

"Kutokana na bidii ya wanajeshi wa Iraq, wanaoshirikiana bega kwa bega na Wamarekani kwenye maeneo ya kivita. Kuna hatua za usalama mbalimbali ambazo Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani na serikali ya Iraq watatekeleza ili kufikia lengo letu la pamoja: kuzuia wale ambao wana mpango wa uhalifu au wa kigaidi kuingia Marekani Marekani. Nataka kutoa shukrani zangu kwa Waziri Mkuu al-Abadi kwa msaada wake na juhudi katika utekelezaji wa hatua hizi, " amesema Wazziri wa mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson.

Wananchi wa Iran, Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen, hata hivyo wamepigwa marufuku kuingia nchini Marekani kwenye agizo hili jipya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.