Pata taarifa kuu
MAREKANI-SIASA

Rais Trump awakwepa wanahabari anapotimiza siku 100 madarakani

Rais wa Marekani Donald Trump ameadhimisha siku 100 madarakani kwa kukutana na kuwahotubia wafuasi wake katika jimbo la Pennsylvania.

Rais wa Marekani akizungumza na wafuasi wake mjini Pennsylvanie
Rais wa Marekani akizungumza na wafuasi wake mjini Pennsylvanie REUTERS/Carlo Allegri
Matangazo ya kibiashara

Mwandishi wa RFI jijini Washington DC, Anne-Marie Capomaccio ameripoti kuwa, Trump ameadhimisha siku 100 madarakani kwa njia tofauti na watangulizi wake ambao wamekuwa wakitumia siku hiyo kwa kukutana na wanahabari katika Ikulu ya Marekani na kuzungumzia changamoto zinazowakabili.

Hata hivyo, wanahabari nchini humo walindaa hafla yao licha ya rais Trump kuisusia, ikiwa ni ishara ya uhusiano mbaya kati yake na wanahabari nchini humo.

Miaka iliyopita, pamoja na kukutana na kuzungumzia maswala mbalimbali, waandishi wa Habari wamekuwa wakipata fursa katika miaka iliyopita, kumuuliza rais maswala ya kitaifa na kimataifa.

Wanahabari nchini Marekani hata hivyo wamesema kuwa, walitumia siku hizo kutafakari taaluma yao wala sio uongozi wa rais Trump.

Shirika la Kimataifa la kutetea maslahi ya wanahabari RSF limesema uhuru wa wanahabari umeshuka sana kwa kipindi cha siku 100 ambacho rais Trump amekuwa uongozini.

Yote haya yanajiri wakati huu wanahabarti wakitarajiwa kuadhimisha siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya Habari tarehe 3 mwezi Mei.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.