Pata taarifa kuu
MAREKANI

Mwanasheria mkuu wa Marekani matatani kwa kudanganya

Mwanasheria mkuu wa Marekani, Jeff Sessions, alikutana kwa zaidi ya mara mbili na balozi wa Urusi wakati wa kampeni za urais za Donald Trump mwaka uliopita, Serikali imethibitisha.

Mwanasheria mkuu wa Marekani, Jeff Sessions ambaye sasa anadaiwa alidanya kuhusu mkutano wake na balozi wa Urusi.
Mwanasheria mkuu wa Marekani, Jeff Sessions ambaye sasa anadaiwa alidanya kuhusu mkutano wake na balozi wa Urusi. REUTERS/Kevin Lamarque/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Sessions ambaye wakati huo alikuwa ni seneta, hakuweka wazi mkutano wake na balozi wa Urusi wakati alipohojiwa na wabunge wakati wa kuthibitishwa kwake kama mwanasheria mkuu.

Hata hivyo amesisitiza kuwa hakuwahi kukutana na kiongozi yeyote wa Urusi kuzungumzia masuala ya kampeni.

Kiongozi wa wachache bungeni kutoka chama cha Democrats, Nancy Pelos, amemtumu Sessions kwa kudanganya wakati akiwa chini ya kiapo na kumtaka ajiuzulu nafasi yake.

Wabunge wengine wamemtaka aachie nafasi yake kupisha uchunguzi wa shirika la upelelezi FBI, ambalo linamchunguza mwanasheria mkuu kuhusu madai haya mapya dhidi yake.

Taarifa hizi zimeibuka punde tu baada ya bunge la Congress kukubali kufanyike uchunguzi rasmi kuhusu madai kuwa Urusi iliingia uchaguzi wa nchi hiyo kwa kufanya udukuzi.

Kamati ya masuala ya intelijensia inatarajia kuwachunguza na kuwahoji maofisa wa Serikali ya Trump pamoja na watu wake wa kampeni kuhusiana na kufanya mawasiliano na Urusi.

Ikulu ya Marekani yenyewe imekanusha kuwepo kwa mgongano wowote wa kimaslahi wala jambo baya lililofanywa wakati wa kampeni za urais mwaka uliopita.

Hata hivyo nchi ya Urusi imeendelea kukanusha shutuma zinazoelekezwa dhidi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.