Trump amshtumu Obama kuchochea vurugu Marekani
Rais wa Marekani Donald Trump anasema anaamini kuwa mtangulizi wake Barrack Obama, anachochea maandamano yanayojitokeza kupinga hatua yake ya kutaka wahamiaji kutoka mataifa saba ya Kiislamu wasije Marekani kwa sababu za kiusalama.
Imechapishwa:
Trump amelimbia Shirika la Habari la Fox News kwamba ana imani kuwa Obama anahusika kwa njia moja ama nyingine sababu ni watu wake wanaohusika kwenye maandamano hayo, huku akiongeza kwamba pingamizi dhidi yake ni kwa sababu za kisiasa.
Rais Donald Trump amesema anaamini kuwa Barack Obama ndiye anahusika na maandamano dhidi ya uongozi wa Republican.
Obama hajamjibu Trump kuhusu madai haya.
Bush akosoa maamuzi ya kwanza ya Trump
Rais wa zamani wa Marekani George W. Bush, alifanya mahojiano na kituo cha habari cha NBCna kukosoa maamuzi ya kwanza ya rais wa sasa wa Marekani.
Katika kipindi cha miaka minane iliyopita, rais wa zamani alijizuia kumkosoa mrithi wake, Barack Obama. Hata hivyo ameamua kumkosa kwa Rais Donald Trump. Bila hata hivyo kumtaja jina, rais wa zamani wa Marekani amesema kuwa ana imani na vyombo vya habari ambavyo, kwa upande wake, vinadumisha na kuhimiza wananchi kujua misingi ya demokrasia.
Amebaini kinyume na alivyosema Trump, kwamba vyombo vya habari si maadui wa Marekani.
Trump kulihutubia taifa Jumanne hii
Siku arobaini baada ya kuchukua hatamu ya uongozi wa nchi, Donald Trump atalihutubia taifa Jumanne hii, Februari 28 bele ya Bunge na Baraza la Seneti.
Itakua ni mara ya kwanza Rais Donald trump kulihutubia taifa toka kutawazwa kwake.