Pata taarifa kuu
MAREKANI-MAUAJI-USALAMA

Mageuzi ya msamaha wa viza yapitiwa katika Baraza la wawakilishi Marekani

Baraza la Wawakilishi limepitisha Jumanne hii kwa idadi kubwa uamzi wa kuimarisha udhibiti kwa raia wa nchi 38 wanaohitaji viza ya kuingia nchini Marekani.

Wabunge wa Marekani wamepitisha Jumanne hii kwa idadi kubwa uamzi wa kuimarisha udhibiti kwa raia wa nchi 38 wanaohitaji viza ya kuingia nchini Marekani.
Wabunge wa Marekani wamepitisha Jumanne hii kwa idadi kubwa uamzi wa kuimarisha udhibiti kwa raia wa nchi 38 wanaohitaji viza ya kuingia nchini Marekani. REUTERS/Tony Gentile
Matangazo ya kibiashara

Nakala hii, sehemu ya pili ya kukabiliana na mashambulizi yaliyoendeshwa tarehe 13 Novemba mjini Paris na Saint-Denis, imepitishwa kwa kura 407 dhidi ya 19.

Nakala hii inaamuru wasafiri wanaohitaji viza kwa sababu ya uraia wao kupata kuruhusiwa mara moja kuingia Marekani kama walikwenda Syria, Iraq, Iran au Sudan katika kipindi cha miaka mitano kabla ya ziara yao.

"Sheria hii itasaidia kuziba pengo katika mdororo wa usalama na kuboresha uwezo wetu wa kuzuia watu hatari kufikia eneo letu", amesema Michael McCaul, mbunge kutoka chama cha Republican, mwenyekiti wa Kamati ya Usalama wa ndani katika Baraza la Wawakilishi.

Wageni milioni ishirini huingia kila mwaka nchini Marekani kwa viza maalum "Visa Waiver Program", ambayo inawaruhusu kukaa siku 90.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.