Pata taarifa kuu
MAREKANI-MAUAJI-USALAMA

Obama: "sababu za shambulizi bado hazijajulikana"

Rais wa Marekani Barack Obama amesema Alhamisi hii kuwa sababu za wahusika wa shambulizi lililogharimu maisha ya watu wengi katika kaunti ya San Bernardino (California) Jumatano usiku wiki hii zilikua bado hazijajulikana, akisema kwamba kuna uwezekano kuwa shambulizi hio lilikua la kigaidi.

Rais Barack Obama akielezea kukerwa na mashambulizi ya mara kwa mara Marekani.
Rais Barack Obama akielezea kukerwa na mashambulizi ya mara kwa mara Marekani. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

"Katika hatua hii hatujajua ni kwa nini tukio hili la kutisha liilitokea", Obama amesema kutoka Ikulu ya White House ambapo lilikuwepo baraza la kitaifa la usalama.

"Tunajua kwamba watu wawili ambao waliuawa walikuwa walijihami kwa silaha na inaonekana kuwa walikua na silaha nyingine katika nyumba zao", Rais Obama ameonge. "Lakini hatujui ni kwa nini walifanya hivyo, hatujui nia yao."

"Inawezekana kwamba shambulizi hili linahusiana na ugaidi, lakini hatujui. Inawezekana pia kwamba shambulizi hili linahusiana na mahali pa kazi", aliendelea Rais Obama, akiongeza kuwa FBI ilikuwa imeanzisha uchunguzi.

Shambulizi hili, ambalo liligharimu maisha ya watu wasiopungua 14, lilifanywa na watu wawili ambao walikua walijihami kwa silaha kubwa, ambao waliuawa na polisi muda mchache baadae.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.