Pata taarifa kuu
MAREKANI-SHAMBULIO-USALAMA

Marekani: watu kumi wauawa katika Chuo Kikuu cha Oregon

Mtu mwenye silaha ameendesha shambulio katika chuo kikuu cha Umpqua Community College karibu na Kaunti ya Roseburg, katika jimbo la Oregon katika pwani ya magharibi ya Marekani, Alhamisi saa 4:40 saa za Marekani (sawa na 11:40 saa za kimataifa).

Katika chuo kikuu cha Umpqua Community College, baada ya shambulio lililowaua watu kumi, Oktoba 1, 2015.
Katika chuo kikuu cha Umpqua Community College, baada ya shambulio lililowaua watu kumi, Oktoba 1, 2015. REUTERS/Michael Sullivan/The News-Review
Matangazo ya kibiashara

Polisi imesema watu kumi wameuawa katika shambulio hilo na zaidi ya 20 wamejeruhiwa. Kijana wa umri wa miaka 20, aliyeendesha shambulio hilo alipigwa risasi na polisi wa Oregon.

" Mtu aliyeendesha shambulio hilo ameuawa ", amesema mkuu wa Kaunti ya Oregon, Sheriff John Hanlin, wakati wa mkutano na waandishi wa habari, bila hata hivyo kuthibitisha idadi ya watu ya kumi waliouawa na zaidi ya 20 waliojeruhiwa, idadi ambayo imetolewa na vyombo vya habari.

Askaeri polisi walipowasili katika chuo kikuu Umpqua Community College walirushiana risasi na kijana huyo aliyeendesha shambulio hilo, na muda mfupi baadaye kijana huyo aliuawa", ameongeza John Hanlin.

Muuaji ajulikana

Katika mazungumzo ya nambari ya dharura (911) yaliyorekodiwa na kurushwa hewani na vyombo vya habari vya Marekani, inasikika kuwa muuaji aliingia darasa kwa darasa, kabla kurushiana risasi na askari polisi waliofika eneo la tukio kwa mara ya kwanza. Pia aliwauliza wanafunzi waliokuwepo eneo hilo kila mmoja kutaja dini yake kabla ya kuwafyatulia risasi.

Muuaji "amejulika", mkuu wa polisi katika Kaunti ya Oregon amethibitisha, bila hata hivyo, kutaja jina lake. Kama bado hatujajua lengo la muuaji huyo, lakini tunajua kwamba kitendo chake kiliandaliwa na onyo lilirushwa kwenye mitandao ya kijamii. Taarifa hizi zinatakiwa kuthibitishwa.

Haijulikani kama mtu huyu alikuwa washirika wala malengo yake hayajulikani. Haijulikani kama muuaji huyo alikuwa mwanafunzi, mwalimu au mtu mwengine aliyepenya na kuingia katika chuo hicho. Pia haijulikani nisilaha ipi ilitumiwa kwa kuendesha shambulio hilo.

Eneo hilo limezingirwa. Vikosi vya usalama vimezingira mabweni na majengo ya chuo kikuu hicho ili kuhakikisha kwamba usalama umeimarishwa eneo hilo, lakini pia kuchunguza iwapo hakuana mwathirika aliyebaki katika eneo hilo la tukio.

Rais wa Marekani Barack Obama amelaani shambulio hilo na kusema kuwa waliotekeleza shambulio hilo walifanya kitendo cha ujinga kisiokua na faida yoyote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.