Pata taarifa kuu
MAREKANI-IS-USALAMA

Barack Obama aahidi "kuliangamiza kundi la IS"

Rais wa Marekani Barack Obama, ameahidi akiwahakikishia raia wake baada ya mauaji yaliotokea Jumatano juma lililopita katika kituo cha kijamii cha San Bernardino, katika jimbo la California, kwamba yuko tayari kulitokomeza kundi la Islamic State.

Rais Barack Obama katika taarifa kuhusu mashambulizi katika mji wa Paris Novemba 13, 2015 katika Ikulu ya White House mjini Washington.
Rais Barack Obama katika taarifa kuhusu mashambulizi katika mji wa Paris Novemba 13, 2015 katika Ikulu ya White House mjini Washington. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

"Tutalitokomeza kundi la (IS)", Rais Barack Obama ameahidi, Jumapili, Desemba 6, katika hotuba yake kwa taifa.

Watu kumi na wanne waliuawa kwa risasi na wanandoa ambao walidaikuwa wafuasi wa kundi la Islamic State (IS). Kundi hili la kiislamu lilikaribisha Jumamosi Desemba 5 uhalifu uliotekelezwa na "wafuasi" wake.

"Hiki ni kitendo cha ugaidi", ameelezea rais Obama, akikumbusha hata hivyo kwamba hakuna ushahidi wowote unaoonyesha "wauaji" walikuwa wakiongozwa na kundi kutoka nje ya nchi. "Lakini ni wazi kwamba watu hawa wawili walikuwa walifuata njia ya msimamo mkali", rais Obama ameongeza kabla ya kutoa wito kwa Waislamu kupambana na "watu wenye msimamo mkali wa kiitikadi". Pia ameyataka makampuni mashuhuri katika teknolojia kuunganisha nguvu zao na zile za mamlaka, wakati ambapo propaganda za kundi la IS zina nguvu kubwa hasa kwenye mitandao ya kijamii.

Rais, ambaye tayari ameonyesha mara kadhaa nia yake ya kudhibiti silaha za moto katika nchi yake, amesema angeweza kuuliza Baraza la Wawakili kupiga kura kwa ajili ya watu binafsi kupigwa marufuku ya kusafiri kwa ndege. Amehakikisha haja ya udhibiti wa silaha ndogo ndogo: wauaji wa San Bernardino ambao kwa urahisi na kisheria wameweza kuwa na silaha nyingi.

"Marekani haitaruhusu wanajeshi wake kuanzisha vita vya aridhini nchini Iraq na Syria", amesema rais Barack Obama. Muungano unaoongozwa na Marekani unaendesha mashambulizi ya anga dhidi kundi la Islamic state nchini Syria na Iraq kwa zaidi ya mwaka. Ikulu ya Marekani, hata hivyo, iko tayari kupeleka wanajeshi zaidi nchini Iraq na Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.