Pata taarifa kuu
DUNIA-MALARIA-AFYA

Vita dhidi ya ugonjwa wa Malaria kutatizwa na janga la Covid-19

Ulimwengu unaadhimisha leo Jumamosi Aprili 25 Siku ya Kimataifa ya kupiga vita dhidi ya ugonjwa wa Malaria. Ugonjwa huo uliathiri watu milioni 228 mwaka 2018 na kuuwa watu 405,000.

Kampeni ya chanjo dhidi ya Malaria katika hospitali ya uzazi ya Ewin Polyclinic huko Cape Coast, Ghana, Aprili 30, 2019.
Kampeni ya chanjo dhidi ya Malaria katika hospitali ya uzazi ya Ewin Polyclinic huko Cape Coast, Ghana, Aprili 30, 2019. CRISTINA ALDEHUELA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mwaka huu inatabiriwa kuwa idadi ya wagonjwa wa Malaria na vifo kutokana na ugonjwa huo inaweza kuwa kubwa zaidi kutokana na janga la Covid-19.

Zaidi ya watu 700,000 wamefariki dunia kwa ugonjwa wa malaria mnamo mwaka 2020. Hizi ni takwimu za Shirika al Afya Duniani (WHO) ikiwa mipango ya kuzuia ugonjwa huo itatatizwa na janga la Covid-19.

Pamoja na 93% ya kesi za ugonjwa huo na 94% ya vifo, bara la Afrika liko katika mazingira magumu.

"Afrika ilipiga hatua kubwa katika miaka 20 iliyopita," amesema Dk Moeti, Mkurugenzi wa Shirika al Afya Duniani katika kanda ya Afrika.

"Ingawa Covid-19 ni tishio kubwa kwa afya, ni muhimu kudumisha mipango ya kuzuia ugonjwa wa malaria na matibabu. Hatupaswi kurudi nyuma,” ameongeza Mkurugenzi wa Shirika al Afya Duniani katika kanda ya Afrika.

"Hatujafikia kwenye hatua tunayotaka," amesema Dk Spès Ntabangana, anayehusika na mkakati pamoja na ufuatiliaji na tathmini kwa shirika la Afya Duniani katika kanda ya Afrika ya Kati.

"Mnamo mwaka wa 2018, ni 50% tu ya raia ambao walitumia vyandarua. Wanawake wajawazito ambao wanapaswa kupokea dozi tatu za sulfadoxine pyrimethamine wakati wa ujauzito, walikuwa 31% tu ambao walifanya hivyo. Sehemu kubwa ya watoto walio na dalili za ugonjwa wa Malaria hawajapata huduma yoyote ya matibabu. Mnamo mwaka 2018 walikuwa zaidi ya theluthi moka," amesema Dk Spès Ntabangana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.