Pata taarifa kuu
AFRIKA-CORONA-AFYA-UCHUMI

Ripoti ya Benki ya Dunia: Mataifa mengi ya Afrika yataathirika kiuchumi kufuatia ugonjwa wa Covid-19

Benki ya Dunia inasema uchumi katika mataifa mengi ya bara la Afrika, utayumba kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona mwaka huu wa 2020 kwa mara ya kwanza baada ya miaka 25.

Mataifa mengi barani Afrika yanaendelea kuathirika kiuchumi kutokana na virusi vya Corona.
Mataifa mengi barani Afrika yanaendelea kuathirika kiuchumi kutokana na virusi vya Corona. REUTERS/Zohra Bensemra
Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya Benki hiyo inaeleza kuwa ukuaji wa uchumi wa mataifa hayo utashuka kwa asilimia 2.1 na kufikia asilimia 5.1.

Mwaka uliopita, uchumi huo uliongezeka kwa asilimia 2.4.

Aidha, ripoti hiyo inaeleza kuwa mataifa hayo yatapoteza kati ya Dola Bilioni 37 hadi Bilioni 79 katika vita dhidi ya virusi hivyo ambavyo vimesabisha kukwama kwa shughuli za kawaida kama biashara na sekta ya utalii.

Kufikia wiki hii, shirika la Afya Duniani, WHO, limeripoti kuwa watu zaidia ya Elfu 10 wamemabukizwa virusi vya Corona barani Afrika huku wengine zaidi ya 500 wakipoteza maisha.

Benki ya dunia na shirika la Afya Duniani, yanasema yanajitahidi kutafuta fedha kuyasaidia mataifa ya Afrika kupambana na janga hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.