Pata taarifa kuu
DRC-MGOMO-AFYA

Madaktari kuendelea na mgomo DRC

Madaktari nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wamesema watarejelea mgomo wa nchi nzima siku ya Jumatatu ijayo Aprili 23 mwaka huu.

Kinshasa, Hospitali ya Cinquantenaire.
Kinshasa, Hospitali ya Cinquantenaire. (Ministère congolais des Affaires étrangères)
Matangazo ya kibiashara

Jopo la madaktari limetoa tangazo Alhamisi wiki hii kuwa hatua zote zimefuatwa, na kwamba Waziri Mkuu wa nchi hiyo Bruno Tshibala amepewa barua yenye mapendekezo yaliyokubaliwa na pande zote mbili, lakini hakuna majibu yoyote ametoa.

Madaktari wanadai nyongeza ya mishahara yao pamoja na malipo ya ziada wanapofanya kazi katika mazingira hatarishi.

Licha ya kutanganzwa mgomo huo, madaktari wamesema kuanzia siku ya Jumatatu ambao watapewa matibabu ni wagonjwa wa dharura pekee na wale waliolazwa hospitalini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.