Pata taarifa kuu
DRC-CENI-UCHAGUZI-SIASA

Watu 267, 000 kukabiliwa na sheria kwa kujiandikisha zaidi ya mara DRC

Tume ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imewafungulia mashtaka watu 267,000 waliobainika kujiandikisha zaidi ya mara moja wakati wa zoezi la kuwasajili wapiganaji kura mwaka uliopita, kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Desemba.

Tume ya Uchaguzi DRC (CENI) imeonya watu watakaopatikana wakijiandikisha zaidi ya mara moja, kwa mijali ya kupata kadi ya kupigia kura, watachukuliwa hatua za kisheria.
Tume ya Uchaguzi DRC (CENI) imeonya watu watakaopatikana wakijiandikisha zaidi ya mara moja, kwa mijali ya kupata kadi ya kupigia kura, watachukuliwa hatua za kisheria. MONUSCO/Florence Marchal
Matangazo ya kibiashara

Akiwa mjini Bukavu mapema Juma hili Naibu Mwenyekiti wa CENI, Norbert Basangezi alionya kwa watu watakaopatikana wakijiandikisha zaidi ya mara moja kwa minajili ya kupata kadi ya kupiga kura, sheria itafuata mkondo wake.

"Mtu yeyote ambaye ataonekana amejirodhesha mara mbili au mara tatu katika vituo vyetu [ili kupata kadi ya kupiga kura] atafikishwa mbele ya mahakama," Naibu Mwenyekiti wa CENI, Norbert Basengezi, alionya.

Hayo yanajiri wakati ambapo Tume ya Uchaguzi nchini DRC (CENI) ilisema kuna umuhimu wa kutumia mashine za kupigia kura katika uchaguzi ujao uliopangwa kufanyika Desemba 23.

Hivi karibuni upinzani ulitishia kutoshiriki uchaguzi iwapo mashine hizo zitatumika kwa uchaguzi huo.

Bw Nangaa amesema uchaguzi unaweza kufanyika hata kama upinzani utakua umesusia.

Uchaguzi nchini DRC umepangwa kufanyika Desemba 23 mwaka huu, lakini sintofahamu imeendelea kuhusu uchaguzi huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.