Pata taarifa kuu
SOMALIA-UKAME

Rais wa Somalia atangaza janga la kitaifa kutokana na ukame

Rais mpya wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed ametangaza hali ya ukame nchini humo kuwa janga la kitaifa.

Rais mpya wa Somalia  Mohamed Abdullahi Mohamed.
Rais mpya wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed. REUTERS/Ismail Taxta
Matangazo ya kibiashara

Somalia inaungana na Sudan Kusini ambayo tayari kiongozi wake Salva Kiir ametangaza hali hiyo.

Kiongozo huyo mpya wa Somalia ambaye anafahamika kwa jina maarufu la Farmajo, ameitaka Jumuiya ya Kimataifa kuwasadia raia wake wanaoendelea kuteseka kwa sababu ya ukosefu wa chakula na maji.

Hali hiyo imesababisha maelfu ya raia wa nchi hiyo hasa watoto kusumbuliwa na tatizo la utapia mlo, huku Shirika la afya duniani WHO likisema kuwa nchi hiyo inapitia hali mbaya ya ukame kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 25.

Raia wa Somalia wapatao Milioni 6 na Laki Mbili wanahitaji misaada ya kibinadamu kwa haraka huku wengine zaidi ya Milioni tatu wakiendelea kukabiliwa na baa la njaa kila siku.

Mabadiliko ya hali ya hewa lakini mashambuliizi ya kigaidi yanaelezwa kuwa sababu kubwa ya kusababisha hali hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.