Pata taarifa kuu
SOMALIA-UCHAGUZI-SIASA

Rais mpya wa Somalia aahidi kuboresha usalama wa nchi na maridhiano

Sherehe ya kuapishwa kwa Rais wa Somalia Abdullahi Mohamed Farmajo imefanyika Jumatano wiki hii katika mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu.

Wakati wa sherehe ya kuapishwa kwa rais Farmajo, mitaa kadhaa ilifungwa huku shule na maduka pia vikifungwa. Wakati huo huo safari za ndege za kibiashara zilifutwa.
Wakati wa sherehe ya kuapishwa kwa rais Farmajo, mitaa kadhaa ilifungwa huku shule na maduka pia vikifungwa. Wakati huo huo safari za ndege za kibiashara zilifutwa. REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Marais wa Djibouti Ismail Omar Guelleh na Uhuru Kenyatta wa Kenya na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn waliwasili kuhudhuria sherehe hiyo tangu asubuhi. Viongozi wengine wa kikanda walikua wanatarajiwa, kama vile ujumbe kutoka Kuwait na Misri.

Kulingana na wachambuzi, changamoto nyingi zinaisubiri serikali mpya, Ikiwa ni pamoja na mapambano dhidi ya wapiganaji wa jihadi wa kundi la Al-Shabab na ukame mkali ambao unaiweka nchi hiyo hatarini kwa baa la njaa.

Mjumbe maaalum wa Umoja wa Mataifa kwa Somalia Michael Keating amesema ni wakati muhimu kwa nchi hiyo kuwa na maendelea katika nyanja mbalimbali.

Katika hotuba yake, Rais mpya Mohamed Abdullahi Farmajo, ameahidi kuboresha usalama wa nchi na kufanya kazi kwa minajili ya kuborsha maridhiano.

Mji wa Mogadishu ulikumbwa tena Jumatano na hatua kali za kiusalama kwa ajili ya kutawazwa kwa Rais mpya wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed.

Mitaa kadhaa ilifungwa huku shule na maduka pia vikifungwa. Wakati huo huo safari za ndege za kibiashara zilifutwa.

Farmajo alichukua hatamu ya uongozi tarehe 16 Februari 2017. Sherehe ya kukabidhiana madaraka ilikumbwa na urushwaji wa mabomu ambayo yalidaiwa kutekelezwa nakundi la Al Shabab karibu na ikulu ya rais, shambulizi ambalo liligharimu maisha ya watu watano, ikiwa ni pamoja na watoto wawili.

Tangu kuanguka kwa utawala wa rais Siad Barre mwaka 1991, Somalia imekuwa katika machafuko na vurugu,yanayosababishwa na wanamgambo wa kiukoo, makundi ya uhalifu na makundi ya Kiislam.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.