Pata taarifa kuu

Mawaziri wa Ulinzi wa Burkina Faso na Côte d'Ivoire wajadili usalama na ushirikiano

Waziri wa Burkina Faso mwenye dhamana ya Ulinzi, Jenerali Kassoum Coulibaly na mwenzake wa Côte d'Ivoire, Téné Birahima Ouattara, walikutana jana (Ijumaa). Walizungumza haswa juu ya ushirikiano wa kijeshi. Mwishoni mwa mkutano huu, wajumbe hao wawili waliondoka wakiwa na matumaini, wakitumai kuwa uhusiano kati ya nchi zao mbili utaimarika.

Niangoloko, mji wa mwisho nchini Burkina Faso kabla ya mpaka na Côte d'Ivoire.
Niangoloko, mji wa mwisho nchini Burkina Faso kabla ya mpaka na Côte d'Ivoire. Google Maps
Matangazo ya kibiashara

Mkutano uliandaliwa chini ulinzi mkali, kimebaini chanzo ckutoka Côte d4ivoire. Mkutano huo ulifanyika Niangoloko, mji wa Burkina Faso karibu na mpaka.

Mwishoni mwa mkutano wao, maofisa hawa wawili walionekana kuwa na matumaini, wakizungumza juu ya "udugu" unaounganisha nchi zao mbili. "Tunatumai kuanza upya, kupambana vilivyo dhidi ya ugaidi na aina mbalimbali za usafirishaji haramu wa binadamu katika mipaka yetu," alisema Jenerali Kassoum Coulibaly, Waziri wa Ulinzi wa Burkina Faso. "Tumepitia pointi zote za uhusiano kati ya nchi hizo mbili," alisema Téné Birahima Ouattara, Waziri wa Ulinzi wa Côte d'Ivoire, bila kuingia kwa undani.

Suala la doria mseto mpakani, zilizositishwa kwa miezi kadhaa, litaweza kushughulikiwa. Kama tu lile la kuvuka mpaka, ambalo lilisababisha kukamatwa kwa askari wawili wa Côte d'Ivoire waliokuwa wa kikosi cha Bouna mwezi Septemba mwaka uliyopita (baada ya kupotea kwenye eneo la uchimbaji haramu wa dhahabu upande wa Burkina Faso), kisha, mwishoni mwa mwezi Machi, askari mmoja na msaidizi mmoja wa kiraia wa Burkina Faso waliokamatwa nchini Côte d'Ivoire.

"Tukio la aina hii linapotokea, tunapata uwezo fikra mbalimbali tena muhimu kati yetu kuweza kulitatua," Amadou Coulibaly, waziri na msemaji wa serikali ya Côte d'Ivoire, alisema Jumatano, akionyesha matokeo mazuri kwa masuala haya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.