Pata taarifa kuu

Mayotte yazindua operesheni mpya dhidi ya ukosefu wa usalama na uhamiaji haramu

Operesheni mpya dhidi ya ukosefu wa usalama, uhamiaji haramu na makazi yasiyo ya usafi imezinduliwa leo Jumanne Aprili 16 huko Mayotte, mwaka mmoja baada ya kuanza operesheni ya kwanza inaoitwa "Wuambushu", imetangaza Wizara ya Ufaransa yenye dhamana ya wilaya za Ng'ambo.

Askari wakimkagua kijana huyu wakati wa operesheni ya usalama katika mji wa Koungou kwenye kisiwa cha Ufaransa cha Mayotte katika Bahari ya Hindi, Februari 16, 2024.
Askari wakimkagua kijana huyu wakati wa operesheni ya usalama katika mji wa Koungou kwenye kisiwa cha Ufaransa cha Mayotte katika Bahari ya Hindi, Februari 16, 2024. © Julien de Rosa / AFP
Matangazo ya kibiashara

Askari 1,700, polisi na askari lwatashirikishwa kwa ajili ya operesheni hii, inayoitwa "Mayotte place nette" na ambayo inapaswa kudumu kwa wiki 11.

Waziri mwenye dhamana ya Maeneo ya ng'ambo Marie Guévenoux amebainisha kuwa maafisa wa polisi 1,700, askari na wanajeshi watahamasishwa wakati wa operesheni hiyo inayotarajiwa kudumu kwa wiki 11.

Mwaka mmoja baada ya kushindwa kwa Operesheni "Wuambushu", serikali sasa inaweka ina imani na kikosi hiki kitakachoendesha operesheni hii ili kukomesha ghasia ambazo zinayumbisha Mayotte. Katika mahojiano na televisheni France 2 kwenye kipindi cha "Télématin" leo Jumanne, Mjumbe wa Waziri wa Maeneo ya Ng'ambo, Marie Guévenoux, ametangaza uzinduzi wa operesheni ya "Mayotte place nette". "Tangu alfajiri ya leo asubuhi huko Mayotte, operesheni mbili, moja ya polisi na moja ya askari wa jeshi, imekuwa ikifanyika, katika maeneo mawili tofauti kisiwani humo. [...] Asubuhi ya leo, kuna maofisa wa polisi 400 na askari polisi,” amesema.

"Mayotte ni Jamhuri"

Ingawa jina limebadilika, malengo yamebaki sawa. "Kupambana dhidi ya uhamiaji haramu, kupambana na viongozi wa magenge, kupambana dhidi ya makazi yasiyo safi," amesema waziri huyo. Mbali na kulenga "viongozi 60 wa magenge", operesheni hiyo inalenga kuharibu makazi 1,300 yasiyo safi, "mara mbili ya operesheni ya mwaka jana", lakini pia mfumo ulioimarishwa dhidi ya uhamiaji haramu. Ndege ya kiraia itapaa juu ya kisiwa hicho wakati wa operesheni ili kuangalia mienendo ya wahamaji baharini. Kwa kuongeza, "meli ya bahari kuu" itakuwa na jukumu la "kukata njia ya wahamiaji kwenda nchi za Maziwa Makuu" kwenye Mto wa Msumbiji na "boti mbili za kijeshi utahusika na kuwakamata wahamiaji xanaojaribu kutoroka baharini". Hatimaye, brigedi za vikosi vya ardhini zitaenda kwenye "vituo vya mbalimbali baharini kukabiliana dhidi ya uhamiaji haramu," ameongeza Marié Guévenoux. "Lazima tuonyeshe kwamba Mayotte ni Jamhuri," amresema Waziri wa Maeneo ya Ng'ambo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.