Pata taarifa kuu

Paris yatayarisha kusitisha sheria ya ardhi kwa kisiwa cha Ufaransa cha Mayotte

Kisiwa cha Ufaransa cha Mayotte, katika Bahari ya Hindi, bado kinakabiliwa na sintofahamu siku ya Jumatatu kutokana na wakazi waliokasirishwa na ukosefu wa usalama na uhamiaji usiodhibitiwa, licha ya tangazo la serikali siku moja kabla kuhusu mipango ya kukomesha haki ya ardhi ili kupunguza shinikizo la wahamiaji.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Gérald Darmanin anataka kukomesha haki ya ardhi: "Haitawezekana tena kuwa Mfaransa ikiwa wewe si mtoto wa wazazi wenye uraia wa Ufaransa."
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Gérald Darmanin anataka kukomesha haki ya ardhi: "Haitawezekana tena kuwa Mfaransa ikiwa wewe si mtoto wa wazazi wenye uraia wa Ufaransa." © AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Rais Emmanuel Macron anawapokea mawaziri wanaohusika Jumatatu alasiri kujadili mageuzi ya katiba ambayo yanapaswa kuondoa haki hii katika kisiwa hicho, ambapo anatuhumiwa kupendelea makazi ya wahamiaji haramu hasa kutoka nchi jirani ya Comoro. Hatua hii ya mshtuko ilizinduliwa Jumapili na Waziri wa Mambo ya Ndani Gérald Darmanin na mjumbe mwenzake wa ng'ambo Marie Guévenoux wakati wa ziara yake huko Mayotte.

Serikali kuu ina nia ya kuanzisha, miaka kadhaa baadaye, marekebisho ya katiba muhimu kufikia hili, jambo ambalo tayari limelaaniwa na mrengo wa kushoto ambao utakataa kuipigia kura. "Tunapaswa kwenda haraka," Waziri wa Sheria Eric Dupond-Moretti alisema siku ya Jumapili. Kwa sababu uwanjani, Mayotte itaedelea kuzuiwa kwa kiasi kikubwa siku ya Jumatatu. Meli zinazounganisha Grande-Terre na Petite-Terre zimesitisha safari zake kutokana na vizuizi vilivyowekwa tangu Januari 22 katika pembe nne za eneo hilo.

"Si suala la kuondoa vizuizi kwa sasa," Safina Soula, kiongozi wa moja ya makundi ya wananchi, aliiambia shirika la habari la AFP Jumatatu asubuhi. "Tumekubaliana na Waziri, tunasubiri hati za maandishi," alisema. "Tunampa hadi Jumatano ili aweze kupokea barua hii (...) tutaona ikiwa yaliyomo yanakidhi matarajio yetu."

Siku ya Jumapili, Gérald Darmanin alibainisha kuwa barua ya kujitolea ingetumwa mwanzoni mwa wiki hii kwa mkusanyiko wa "wadau wote husika", ambao anaongoza vuguvugu, na kwa viongozi waliochaguliwa. "Nilielewa kwamba baada ya kupokea barua hii, vizuizi vya barabarani vingeondolewa," amesema.

"Hakuna Jamhuri tena"

Mayotte, eneo maskini zaidi la Ufaransa, lina wakazi 310,000, kulingana na INSEE, ofisi ya takwimu ya Ufaransa - pengine zaidi kulingana na taasisi ya Hesabu katika eneo hilo - ikiwa ni pamoja na wahamiaji wa Comoro 48% au nchi nyingine. Wengi huwasili kinyume cha sheria katika boti za uvuvi kutoka kisiwa cha Comoro cha Anjouan, umbali wa kilomita 70 tu. Wengi huishi katika “Bangas” (vibanda) visivyo na usafi.

Ili kujaribu kuzuia wimbi hili la wahamiaji haramu, Gérald Darmanin ameamua kufuta sheria ya ardhi, hatua ambayo yeye mwenyewe ameelezea kuwa ni "yenye nguvu, iliyo wazi, na kali". "Haitawezekana tena kuwa Mfaransa ikiwa wewe sio mtoto wa wazazi wenye uraia wa Ufaransa," amebainisha. lakini hatua hii tayari kwa kiasi kikubwa imegawanya upinzani, kulingana na Bw. Darmanin.

"Ili kutatua matatizo ya Mayotte, hatuhitaji Jamhuri kidogo, tunahitaji Jamhuri zaidi, na kwa hivyo hakika sio kitendo cha kudhoofisha sheria ya ardhi," amesema kwenye CNews/Europe 1, Manuel Bompard, mbunge wa chama cha LFI (mrengo wa kushoto wenye msimamo mkali). "Ni mwanzo mzuri kwani tumekuwa tukitoa wito wa kukomeshwa kwa haki za ardhi kwa nchi nzima kwa miaka ishirini," kinyume chake amekariri kwenye kituo cha Franceinfo Jordan Bardella kiongozi wa chama cha Rassemblement national (mrengo wa kulia).

Kumalizika kwa haki za ardhi huko Mayotte kutafanya iwezekane, kulingana na Bw. Darmanin, kuondoa vibali vya makazi vilivyowekwa kwenye eneo, mfumo unaowazuia wenye kibali cha makazi cha Mayotte kuja Ufaransa bara na ambapo makundi ya wakazi wenye hasira wanadai kukandamizwa.

Idadi ya vibali vya kuishi vilivyotolewa Mayotte itapungua kwa 90% kwa hatua hizi mpya na uimarishaji wa kuunganishwa kwa familia unaoruhusiwa na sheria ya hivi karibuni ya uhamiaji, wasaidizi wa waziri wameliambia shirika la habari la AFP. Kuondolewa kwa mfumo huu kutarekodiwa katika mswada wa Mayotte utakaowasilishwa kwa Bunge hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.