Pata taarifa kuu

Côte d'Ivoire: Rekodi za joto huvuruga kilimo

Tangu mwezi wa Januari, Afrika Magharibi imekuwa ikivunja rekodi za joto zinazohusishwa na mfumo wa hali ya hewa ya El Nino: nchini ekodi za joto, rekodi za joto zinzvuruga kilimo, ambacho kinawakilisha robo ya Pato la Taifa na zaidi ya nusu ya ajira.

Baada ya mvua za mwaka jana, wakati huu ni joto kali ambalo linaathiri mavuno nchini Côte d'Ivoire,  mzalishaji mkuu wa kakao duniani (karibu 45%).
Baada ya mvua za mwaka jana, wakati huu ni joto kali ambalo linaathiri mavuno nchini Côte d'Ivoire, mzalishaji mkuu wa kakao duniani (karibu 45%). © AFP
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa miti ya kakao kwenye shamba lake lililo karibu na Agboville, kilomita 70 kutoka Abidjan, Christian André Yapi anagundua kuwa maharagwe hayakui kama kawaida. "Maharagwe yanageuka meeusi", yanaoza na "hayawezi tena kukua kwa sababu ya joto", ameliambia shirikala habari la AFP. Majani ya miti ya kakao kawaida huweka kivuli kwenye maharagwe, lakini jua "huyakausha na kudondoka," anaongeza.

Kwa sababu ya joto, Bw. Yapi anafanya kazi tu asubuhi, na kwa anapopumzika, anahesabu hasara zake. "Katika msimu mfupi, mimi hutengeneza hadi tani moja," anaeleza, akisikitishwa tu na kuzalisha "kilo 300" mwaka huu. Baada ya mvua za mwaka jana, wakati huu ni joto kali ambalo linaathiri mavuno ya Côte d4ivoire, mzalishaji mkuu wa kakao duniani (karibu 45%).

Mwaka huu, "tuliona joto kali katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi mwezi Machi", na "rekodi ya digrii 41 mwezi Februari" huko Dimbokro (katikati), anaripoti Daouda Konate, mkurugenzi wa mamlaka ya hali ya hewa nchini Côte d'Ivoire, Sodexam. Kwa wakati huu wa mwaka, "joto kawaida hutofautiana karibu digrii 35-36," anaongeza.

Joto linazidi Afrika

Kulingana na Daouda Konate, ambaye alikua makamu wa rais wa kwanza wa Afrika wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani miezi michache iliyopita, "mwaka huu ni maalum kwa sababu ya El Niño", hali ya asili ya hali ya hewa ambayo inalingana na ongezeko kubwa la joto la Pasifiki ya Kusini. Lakini joto kali pia husababishwa na "hatua za kibinadamu: matumizi na viwanda vyetu", anahakikisha Nahounou Pierre Lautti Daleba, mwanauchumi na mtaalamu wa masuala ya tabia nchi, mwanachama wa shirika lisilo la kiserikali la Vijana wa Kujitolea kwa Mazingira nchini Côte d'Ivoire.

Ikiwa Afrika inatoa tu 7% ya uzalishaji wa gesi chafu duniani tangu katikati ya karne ya 19, kulingana na ripoti ya 6 ya IPCC, joto linaongezeka kwa kasi zaidi kuliko mabara mengine

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.