Pata taarifa kuu

Nigeria: Ni miaka 10 sasa tangu kutekwa kwa wasichana wa shule 276

Nairobi – Nchini Nigeria, imetia miaka 10 tangu kutekwa kwa wasichana wa shule 276 wa Chibok katika jimbo la Borno Kaskazini mwa Nigeria, na kundi la kigaidi la Boko Haram, baadhi ya wasichana hao, mpaka leo hawajapikana.

Falamo Mall jijini Lagos ikiwa na picha za wasichana wa shule ya Chibok (14/04/2024)
Falamo Mall jijini Lagos ikiwa na picha za wasichana wa shule ya Chibok (14/04/2024) © Abdurrahman Gambo/RFI Hausa (08/12/2023)
Matangazo ya kibiashara

Mashirika ya Kimataifa ya kutetea haki za binadamu yakiongozwa na Amnesty International, yanasema serikali ya Nigeria inapaswa kufanya jitihada za kuhakikisha kuwa wasichana karibu 100 ambao hawajapatikana baada ya kutekwa na Boko Haram, wanaunganishwa tena na familia zao.

Aidha, wanataka ulinzi kuimarushwa kwenye shule hasa Kaskazini mwa Nigeria, ili kuzuia utekwaji wa watoto hasa wanafunzi, jambo ambalo limekuwa likiendelea mara kwa mara tangu sakata la wasichana wa Chibok.

Wazazi wa wasichana waliotekwa nyara wa Chibok wakiwa na picha za binti zao wakati wa kumbukumbu mwaka wa 2019, miaka 10 baada ya kutekwa nyara na Boko Haram.
Wazazi wa wasichana waliotekwa nyara wa Chibok wakiwa na picha za binti zao wakati wa kumbukumbu mwaka wa 2019, miaka 10 baada ya kutekwa nyara na Boko Haram. © AFP

Kwa wazazi ambao hawajawaona wasichana wao, kama Yana Galang, kila siku ni huzuni kwao. Anaishi na matumaini kuwa siku moja, binti yake atapatikana na kurejea nyumbani.

Utekaji wa wanafunzi hao ulishtumiwa na kulaaniwa kote duniani, huku serikali ya Nigeria ikiahidi kuwaokoa wanafunzi hao na kulitokomeza kundi la Boko Haram, lakini miaka 10 baadaye hali imeendelea kuwa mbaya.

Soma piaNigeria: Mmoja wa wasichana wa shule ya upili ya Chibok aachiliwa

Shirika la kimataifa linalotetea haki za watoto la Save the Children, linasema kati ya mwaka 2014 hadi 2022, wanafunzi 1,680 wametekwa na makundi yenye silaha Kaskazini mwa Nigeria.

Hillary Ingati- RFI Kiswahili, Nairobi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.