Pata taarifa kuu

Vifaa vya kijeshi vya Urusi na wakufunzi wawasili Niger

Wakufunzi wa Urusi waliwasili siku ya Jumatano huko Niamey, ambayo pia ilipokea vifaa vya kwanza vya kijeshi vya Urusi kama sehemu ya ushirikiano mpya wa usalama kati ya Niamey na Moscow, televisheni ya umma ya Niger ilitangaza Alhamisi jioni.

Kama Mali na Burkina Faso, Niger imeipa kisogo Paris na ijisogeza karibu zaidi kiuchumi na kijeshi na washirika wapya, ikiwa ni pamoja na Urusi.
Kama Mali na Burkina Faso, Niger imeipa kisogo Paris na ijisogeza karibu zaidi kiuchumi na kijeshi na washirika wapya, ikiwa ni pamoja na Urusi. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Jumatano hii, Aprili 10, 2023, tulishuhudia kuwasili kwa ndege aina ya Iliouchine-76, iliyosheheni vifaa vya hivi karibuni vya kijeshi pamoja na wakufunzi wa kijeshi kutoka Wizara ya Ulinzi ya Urusi," ilitangaza televisheni ya umma Télé Sahel. Shirikisho la Urusi "litaiwezesha" Niger na "kuweka mfumo wa ulinzi wa anga" wenye uwezo wa "kuhakikisha udhibiti kamili wa anga yetu", ilisema televisheni, ikionyesha picha zilizopigwa usiku kutoka kwa ndege kubwa ya Kirusi ilipotua kwenye uwanja wa ndege wa mji mkuu wa Niamey.

Wakufunzi wa kijeshi wa Urusi, ambao idadi yao haikuainishwa, "watatoa mafunzo bora" kwa wanajeshi wa Niger "kwa matumizi bora ya mfumo huo", ilisema televisheni ya umma. "Tuko hapa kutoa mafunzo kwa jeshi la Niger na kulisaidia kutumia vifaa vya kijeshi ambavyo vimewasili hivi punde," mmoja wa wakufunzi wa Urusi alitangaza kwenye runinga hii. "Tuko hapa kuendeleza ushirikiano wa kijeshi kati ya Urusi na Niger."

Mnamo Machi 26, mkuu wa utawala wa kijeshi nchini Niger, Jenerali Abdourahamane Tiani, alizungumza kwa simu na Rais wa Urusi Vladimir Putin kujadili hasa "kuimarishwa" kwa ushirikiano wao wa usalama, taarifa rasmi kwa vyombo vya habari ya Niger ilibaini.

"Wakuu hao wawili wa nchi" walizungumza " juu ya haja ya kuimarisha ushirikiano wa usalama" kati ya Urusi na Niger "kukabiliana na vitisho vya sasa," ilisema taarifa kwa vyombo vya habari, wakati mashambulizi ya wanajihadi yanazorotesha ukanda wa Sahel. Katikati ya mwezi Machi, Niger ilishutumu makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi na Marekani, ikitilia shaka uwepo wa zaidi ya wanajeshi 1,000 wa Marekani nchini Niger.

Niger, kama nchi jirani ya Burkina Faso na Mali, imekuwa ikikabiliwa na ghasia za mara kwa mara na mbaya za wanajihadi kwa miaka mingi, zinazofanywa na makundi ya kijihadi yenye mafungamano na Al-Qaeda na kundi la Islamic State (IS). Katika nchi hizi tatu, serikali za kiraia zimepinduliwa na mapinduzi ya kijeshi mfululizo tangu mwaka 2020.

Kwa kuongezea, makoloni haya matatu ya zamani ya Ufaransa yaliipa kisogo Paris na kujisogeza karibu zaidi kiuchumi na kijeshi na washirika wapya, ikiwa ni pamoja na Urusi, kabla ya kujipanga upya ndani ya Muungano wa Nchi za Sahel (AES) kwa lengo la kuunda shirikisho. Katikati ya mwezi wa Januari, Urusi ilikuwa tayari imetangaza kwamba imekubali "kuimarisha" ushirikiano wake wa kijeshi na Niger. Ujumbe wa Urusi ulikwenda Niamey mnamo mwezi wa Desemba kujadili na jeshi. Makubaliano ya kuimarisha ushirikiano wa kijeshi yalitiwa saini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.