Pata taarifa kuu

Waziri mkuu wa wa Niger Ali Lamine anazuru Moscow

Nairobi – Waziri Mkuu wa Niger Ali Lamine Mahamane Zeine, anazuru Urusi akiwa na ujumbe mkubwa baada ya nchi yake kuwekewa vikwazo vilivyosababisha changamoto za kifedha baada ya jeshi kumwondoa madarakani rais Mohamed Bazoum mwaka uliopita.

Ali Mahamane Lamine Zeine Niger
Ziara hii inalenga kuimarisha uhusiano zaidi na Urusi, baada ya kuonekana kutengwa na mataifa ya Magharibi baada ya mapinduzi ya kijeshi AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Ziara hii inalenga kuimarisha uhusiano zaidi na Urusi, baada ya kuonekana kutengwa na mataifa ya Magharibi baada ya mapinduzi ya kijeshi.

Hii ni mara ya kwanza kwa Waziri Mkuu Zeine, kuzuru Moscow baada ya kuteuliwa, na anaambatana na Waziri wa Ulinzi, Biashara na yule anayehusika na nishati na madini.

Ripoti kutoka Niamey, zinasema Niger inataka ushirikiano wa karibu na Urusi kuhusu masuala ya ulinzi, nishati na kilimo.

Katika mazungumzo yake na Jarida la Sputnik la Urusi, waziri mkuu huyo  amesema ziara hii inalenga pia kuisaidia Niger kwenye mafunzo ya marubani wake na maafisa wa Inteljensia.

Ziara hii inakuja baada ya mwezi Desemba mwaka uliopita, wawakilishi wa mataifa haya mawili kutiliana saini nyaraka za siri kwa mujibu wa ripoti za kidiplomasia, huku kukiwa na maswali iwapo kundi la Wagner linatarajiwa kutumwa nchini Niger.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.