Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-MAANDAMANO

Togo yahirisha uchaguzi wa wabunge hadi Aprili 29

Togo imeahirisha uchaguzi wa wabunge utakaofanyika Aprili 29, baada ya kuahirishwa katika muktadha wa kupitishwa kwa Katiba mpya mwishoni mwa mwezi Machi, ofisi ya rais imetangaza katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa siku ya Jumanne.

Raia wa Togo huhesabu kura wakati wa uchaguzi uliopita nchini Togo, uchaguzi wa urais wa Februari 22, 2020.
Raia wa Togo huhesabu kura wakati wa uchaguzi uliopita nchini Togo, uchaguzi wa urais wa Februari 22, 2020. © Yannick Foly / AFP
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huo ulikuwa ufanyike tarehe 20 Aprili, lakini serikali ya Togo iliahirisha ili kufanya mashauriano kuhusu Katiba mpya, ambayo inachukuliwa na vyama kadhaa vya upinzani kama mbinu ya kumweka Rais Faure Gnassingbé madarakani kwa muda mrefu zaidi. "Tarehe ya uchaguzi wa wabunge na wa magavana: Jumatatu Aprili 29," inaonyesha taarifa kwa vyombo vya habari kutoka ofisi ya rais iliyochapishwa baada ya mkutano wa serikali siku ya .

Vyama vya upinzani havikuitikia mara moja tarehe hii mpya. Mapema siku ya Jumanne, serikali ilipiga marufuku maandamano kwa wito wa vyama vya upinzani kupinga kuahirishwa kwa chaguzi hizi.

Chama cha upinzani cha National Alliance for Change (ANC) na makundi mengine yalijibu marufuku hiyo kwa kuashiria kwamba maandamano bado yatafanyika Ijumaa na Jumamosi. Maandamano kwenye barabara za umma yamepigwa marufuku nchini Togo tangu mwaka 2022, baada ya shambulio katika soko la Lomé ambapo gaskari mmoja alipoteza maisha.

Viongozi wa upinzani wameitaka serikali kubatilisha mageuzi yake ya Katiba ambayo yanaruhusu Bunge kumchagua rais moja kwa moja “bila mjadala”. Rais Gnassingbé amekuwa madarakani tangu mwaka 2005. Alimrithi babake ambaye alitumia karibu miaka 38 akiwa mkuu wa Togo baada ya mapinduzi ya kijeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.