Pata taarifa kuu

Uchaguzi wa Togo waahirishwa kufuatia rasimu ya Katiba mpya

Uchaguzi wa wabunge na wa magavana nchini Togo uliopangwa kufanyika Aprili 20 awali umeahirishwa hadi itakapopangiwa tarehe nyingine, ofisi ya rais wa Togo imetangaza siku ya Jumatano, ikisisitiza haja ya kufanya "mashauriano" juu ya mradi unaopingwa wa mabadiliko ya katiba uliopitishwa mwishoni mwa mwezi wa Machi.

Makao makuu ya Bunge la taifa la Togo, Januari 8, 2019 mjini Lomé.
Makao makuu ya Bunge la taifa la Togo, Januari 8, 2019 mjini Lomé. © Wikimedia Commons CC0 Kayi Lawson (VOA)
Matangazo ya kibiashara

"Serikali itafanya marekebisho madogo ya kalenda ya uchaguzi wa wabunge na wa magavana," imesema taarifa ya ofisi ya rais kwa vyombo vya habari Jumatano, bila kutaja tarehe mpya.

Uamuzi huu unafuatia "ombi la Mkuu wa Nchi Faure Gnassingbé kutaka bunge kuchunguza kwa mara ya pili sheria ya marekebisho ya katiba iliyopitishwa mnamo Machi 25 kwa nia ya mjadala mpya wa Bunge", alielezea rais.

Wiki iliyopita, wabunge wa Togo walipitisha Katiba mpya yenye lengo la kuhamisha nchi kutoka mfumo wa urais hadi mfumo wa bunge.

Marekebisho haya yalipingwa vikali na upinzani na mashirika ya kiraia, ambayo yanaona kama ujanja wa rais kusali madarakani, jambo ambalo lilimsukuma mkuu wa nchi, Faure Gnassingbé, kuomba kura mpya ya wabungesiku chache baadaye.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.