Pata taarifa kuu

Togo: Rais arudisha Katiba mpya bungeni

Mabadiliko nchini Togo: Rais Faure Gnassingbé aliagiza siku ya Ijumaa kwamba Katiba mpya, iliyopitishwa kuanzisha utawala wa bunge na sio tena wa urais, ipelekwe kwa kura mpya ya wabunge, katika mazingira ya mvutano wa kisiasa unaozidi kuongezeka.

Rais wa Togo Faure Gnassingbé wakati wa mkutano wa kilele wa ECOWAS nchini Nigeria, Februari 24, 2024.
Rais wa Togo Faure Gnassingbé wakati wa mkutano wa kilele wa ECOWAS nchini Nigeria, Februari 24, 2024. © AP/Gbemiga Olamikan
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatatu jioni, Bunge, linalotawaliwa na Muungano wa Jamhuri (UNIR), ulio madarakani, liliidhinisha rasimu hiyo mpya, mageuzi ya katiba ambayo yanapingwa vikali na upinzani ambao unaona ni mbinu ya rais kusalia madarakani.

"Kila kitu kikiwa kamilifu, na kwa kuzingatia shauku iliyoamshwa kati ya raia na rasimu hii tangu kupitishwa kwake, rais wa Jamhuri leo amemtaka spika wa Bunge kusoma kwa mara ya pili sheria iliyopitishwa", alitangaza Yawa Kouigan, waziri wa mawasiliano na msemaji wa serikali kwenye televisheni ya taifa Ijumaa jioni.

Tangu kupitishwa kwa Katiba mpya, upinzani umekuwa ukivutana dhidi ya utawala huo, wakihofia kwamba mabadiliko haya yatamwacha wazi Rais Faure Gnassingbé kubaki mkuu wa nchi, wakati uchaguzi wa wabunge na wa magavana utafanyika ndani ya kipindi cha wiki tatu, Aprili 20.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.