Pata taarifa kuu

Upinzani wa Togo kufanya maandamano yaliyopigwa marufuku

Muungano mkubwa wa vyama vya upinzani nchini Togo umeamua siku ya Ijumaa kusisitiza juu maandamano ambayo unaandaa siku ya Jumamosi huko Lomé kupinga kuahirishwa kwa uchaguzi wa wabunge, licha ya maandamano hayo kupigwa marufuku na serikali.

Mikusanyiko ya hadhara inayoandaliwa na upinzani ni nadra na mara nyingi imepigwa marufuku tangu Machi 2020, baada ya kugunduliwa kwa kesi ya kwanza ya UVIKO-19 nchini Togo.
Mikusanyiko ya hadhara inayoandaliwa na upinzani ni nadra na mara nyingi imepigwa marufuku tangu Machi 2020, baada ya kugunduliwa kwa kesi ya kwanza ya UVIKO-19 nchini Togo. © PIUS UTOMI EKPEI / AFP
Matangazo ya kibiashara

 

The Dynamics for the Majority of the People (DMP, muungano wa vyama vya upinzani vya kisiasa na mashirika ya kiraia) wanataka kuandamana dhidi ya "kushindwa kwa serikali kuandaa uchaguzi wa wabunge ndani ya muda uliowekwa na katiba".

Muungano huu pia unapinga, katika taarifa, dhidi ya "kuendelea kuzuiliwa kwa zaidi ya wafungwa mia moja wa kisiasa" na dhidi ya "vikwazo vya uhuru wa umma". Katika barua iliyotumwa kwa waandaaji wa maandamano hayo mnamo Januari 22, Waziri wa Mambo ya Ndani, Kanali Hodabalo Awaté, alitaja sababu za "usalama" hasa.

Alibainisha kuwa maandamano yamepigwa marufuku "tangu shambulio la kigaidi lililotokea katika soko kubwa la Lomé mnamo Juni 2, 2022 na ambalo lilisababisha kifo cha askari na kujeruhiwa vibaya kwa afisa wa polisi aliyekuwa akifanya kazi" . "Maandamano yenu ya siku ya Jumamosi Januari 27, 2024 hayakubaliwi," waziri huyo aliagiza. Maafisa wa DMP walikutana na waziri siku ya Ijumaa lakini walionyesha kuwa msimamo wao haubadiliki, na maandamano yao yanapaswa kufanyika.

Ni hatua zisizofuata msingi wa sheria yoyote. Tutafanya maandamano yetu yaliyopangwa kufanyika Jumamosi huko Lomé," Brigitte Kafui Adjamagbo-Johnson, mratibu wa DMP, ameliambia shirika la habari la AFP. "Hatutashiriki katika ukiukaji wa haki zetu. Kila mtu atatekeleza wajibu wake,” ameongeza.

Mikusanyiko ya hadhara inayoandaliwa na upinzani ni nadra na mara nyingi imepigwa marufuku tangu mwezi Machi 2020, baada ya kugunduliwa kwa kesi ya kwanza ya UVIKO-19 nchini Togo. Uchaguzi wa wabunge na wa magavana, ambao awali ulipangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka 2023, utafanyika "mwisho wa robo ya kwanza ya mwaka 2024", serikali ilitangaza mnamo mwezi wa Novemba 2023. Lakini bado hakuna tarehe iliyopangwa kwa uchaguzi huu kufanyika. Chaguzi za mwisho za wabunge zilifanyika mwaka wa 2018 na zilisusiwa na upinzani ambao ulilaani "mapungufu" katika sensa ya wapiga kura.

Rais Faure Gnassingbé aliingia madarakani mwaka wa 2005 baada ya kifo cha babake, Jenerali Gnassingbé Eyadéma, ambaye alitawala Togo kwa miaka 38. Tangu wakati huo alichaguliwa tena mara tatu katika chaguzi ambazo zote zilipingwa na upinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.