Pata taarifa kuu

Waandishi wawili wa habari wa Togo wafungwa kwa 'kumtusi' waziri

Waandishi wawili wa habari wa Togo wamefunguliwa mashtaka na kufungwa gerezani siku ya Jumatano huko Lomé, wakishutumiwa kwa "kumtusi" waziri mmoja baada ya kudai kwenye mitandao ya kijamii kwamba waziri huyo alizusha kuwa aliibiwa sawa na euro 600,000 nyumbani kwake, ndugu zao wamesema.

Mwezi Machi mwaka jana, waandishi wawili wa habari wa Togo walihukumiwa bila kuwepo mahakamani kifungo cha miaka mitatu jela kwa "kudharau mamlaka" na "kueneza uongo kwenye mitandao ya kijamii".
Mwezi Machi mwaka jana, waandishi wawili wa habari wa Togo walihukumiwa bila kuwepo mahakamani kifungo cha miaka mitatu jela kwa "kudharau mamlaka" na "kueneza uongo kwenye mitandao ya kijamii". © Reuters / Noel Kokou Tadegnon
Matangazo ya kibiashara

Loïc Lawson, mkurugenzi wa uchapishaji wa Gazeti la Flambeau des Démocrates, na Anani Sossou, mwandishi wa habari wa kujitegemea, waliwekwa chini ya ulinzi wa polisi siku ya Jumatatu. Wanashtakiwa kwa "kukashifu na kushambulia heshima ya waziri na kuchochea uasi", kwa kuwa wamethibitisha kwenye mitandao ya kijamii kwamba Waziri wa Mipango Miji, Nyumba na Marekebisho ya Ardhi, Kodjo Adedze, alizusha kuwa aliibiwa nyumbani kwake milioni 400  za faranga za CFA (sawa na euro 604,875).

Waziri ambaye alitangaza wizi huo kwa polisi bila kiasi hicho kuwekwa hadharani, aliwasilisha malalamiko dhidi yao. Wanahabari hao walirejelea madai yao siku ya Jumatatu, wakieleza kwenye mtandao wa Facebook kwamba "uchunguzi wa kina" umeonyesha kuwa "kiasi kilichotangazwa na Waziri kilikadiriwa kupita kiasi na sio jumla yafaranga za CFA milioni 400".

"Waandishi hao wawili waliipelekwa katika gereza (la Lomé) siku ya Jumatano mwendo wa saa nne asubuhi. Walifika mbele ya mwendesha mashitaka Jumanne jioni, ambaye aliwahoji kwa takriban dakika thelathini, kabla ya kuwarejesha kwa kwa mwenzake amabye alichukuwa auamuzi wa kuwapeleka jela," Magloire Têko Kinvi, mhariri mkuu wa Gazeti la Le Flambeau des Démocrates, ameliambia shirika la habari la AFP.

Shirika linalotetea haki za waandishi wa habari, Reporters Without Borders, limetoa wito katika ujumbe uliochapishwa kwenye X (zamani Twitter) ili kuachiliwa mara moja kwa waandishi hao wa habari. 

Nchini Togo, mitandao ya kijamii haijajumuishwa katika wigo wa matumizi ya sheria inayohusiana na kanuni za vyombo vya habari na mawasiliano ambayo yalianza kutumika mwaka huu. Katika tukio la kosa, mashtaka yanatokana na kanuni ya adhabu. Mwezi Machi mwaka jana, waandishi wawili wa habari wa Togo walihukumiwa bila kuwepo mahakamani kifungo cha miaka mitatu jela na mahakama kuu ya Lomé, hasa kwa "kudharau mamlaka" na "kueneza uongo kwenye mitandao ya kijamii", kufuatia malalamiko kutoka kwa mawaziri wawili, akiwemo Bw. Adedze.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.