Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Kesi ya wanajeshi 46 wa Côte d'Ivoire: Gnassingbe aomba msamaha wa rais

Rais wa Togo Faure Gnassingbe amefanya ziara fupi mjini Bamako, Jumatano hii, Januari 4, ili kujadili hatima ya wanajeshi 46 wa Côte d'Ivoire wanaozuiliwa tangu mwezi Julai mwaka jana nchini Mali, faili ambalo Lomé inajaribu kupatanisha.

Askari wa kikosi maalum cha Côte d'Ivoire wakitayarisha risasi zao kwa ajili ya mafunzo.
Askari wa kikosi maalum cha Côte d'Ivoire wakitayarisha risasi zao kwa ajili ya mafunzo. AP - Sylvain Cherkaoui
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi hawa walihukumiwa kifungo cha miaka ishirini jela wiki iliyopita kwa shambulio na kula njama dhidi ya serikali ya Assimi Goïta. Hata kama Faure Gnassingbé alikwepa vyombo vya habari, ziara yake ni hatua muhimu.

Alipowasili, Rais wa Togo Faure Gnassingbé hakutoa taarifa kwa vyombo vya habari. Kulingana na mashahidi, alikimbia haraka kwenye gari akiambatana na rais wa mpito wa Mali, Kanali Assimi Goïta, na hivyo kwenda Koulouba, makao makuu ya ikulu ya rais huko Bamako.

Ilikuwa ni swali la kubaini kile ambacho chanzo kilio karibu na faili hili kimeelezea kama "marekebisho ya mwisho", katika kesi ya wanajeshi 46 wa Côte d'Ivoire waliohukumiwa wiki iliyopita kifungo cha miaka 20 jela nchini Mali.  Kinachotarajiwa ni msamaha unaowezekana wa rais wa Mali, ambao unaweza kusitisha faili hiyo.

Hadi sasa, Togo inapambana na inaendelea kupambana ili kupata matokeo chanya katika kesi hii, na mamlaka ya Mali haifichi ukweli kwamba wanapendelea upatanishi wa Togo kuliko ule wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi, ECOWAS.

Baada ya mkutano huko Koulouba, hakuna kilichovuja kuhusu mazungumzo kati ya viongozi hao wawili. Mashahidi waliowaona wakitoka kwenye jumba hilo wanadai kuwa walikuwa wakitabasamu. Dalili kwa siku zijazo, kwa matokeo ya haraka ili askari wa Côte d'Ivoire wapate uhuru wao kwa msamaha wa rais?

Kwa vyovyote vile, Lomé inalifanyia kazi suala hilo. Mali na Côte d'Ivoire pia. Mahusiano kati ya nchi hizo mbili yameboreka hivi karibuni, kwa kutiwa saini kwa mkataba wa maelewano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.