Pata taarifa kuu

Togo: Wapinzani sita waliokuwa wanazuiliwa Lomé waachiliwa

Wapinzani sita wa Togo waliokuwa wanazuiliwa katika mji mkuu wa Togo, Lomé, tangu siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita kwa "kuhatarisha usalama wa taifa" waliachiliwa Jumanne jioni, ndugu zao wameliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumatano.

Upinzani na mashirika ya kiraia yameitisha maandamano ya siku tatu, Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi kupinga kile wanachoelezea kama "mapinduzi ya taasisi", lakini maandamano haya yamepigwa marufuku na serikali.
Upinzani na mashirika ya kiraia yameitisha maandamano ya siku tatu, Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi kupinga kile wanachoelezea kama "mapinduzi ya taasisi", lakini maandamano haya yamepigwa marufuku na serikali. Matteo Fraschini KOFFI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wanaharakati tisa wa Dynamique Monseigneur Kpodzro (DMK, kundi la vyama vya upinzani na mashirika ya kiraia) walikamatwa walipokuwa "wakhamasisha watu katika soko la Akodessêwa kuhusu marekebisho ya katiba ambayo ni kinume cha sheria", kulingana na DMK.

Rasimu hii ya Katiba mpya, ambayo ingeihamisha Togo kutoka utawala wa rais hadi utawala wa bunge, imeitia wasiwasi nchi hiyo tangu kupitishwa kwake na wabunge mwishoni mwa mwezi Machi, huku upinzani ukiiona kama njia kwa Rais Faure Gnassingbé kubakia madarakani. .Watatu kati ya wale waliokuwa wamefungwa walikuwa tayari wameachiliwa.

"Wanaharakati sita (wa mwisho) wa DMK waliachiliwa siku ya Jumanne jioni na kurudi nyumbani," Thomas Kokou N'soukpoe, msemaji wa DMK, amelithibitishia shirika la habari la AFP. Kwa kujibu wapinzani wake, mkuu wa nchi wa Togo aliomba usomaji mpya wa maandishi yatakayofanywa na Bunge - ambayo tarehe yake bado haijatangazwa - na kuamua kuahirisha uchaguzi wa wabunge na wa magavana kutoka Aprili 20 hadi 29.

Upinzani na mashirika ya kiraia yameitisha maandamano ya siku tatu, Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi kupinga kile wanachoelezea kama "mapinduzi ya taasisi", lakini maandamano haya yamepigwa marufuku na serikali.

Siku ya Jumatano adhuhuri, upinzani ulipanga kudumisha maandamano haya kwa siku mbili za Ijumaa na Jumamosi. Maandamano kwenye barabara za umma yamepigwa marufuku nchini humo tangu mwaka 2022, baada ya shambulio katika soko la Lomé ambapo askari mmoja alipoteza maisha.

Faure Gnassingbé alifika kama mkuu wa nchi mwaka wa 2005, akimrithi baba yake ambaye alisalia madarakani kwa karibu miaka 38. Baadaye alichaguliwa tena katika chaguzi ambazo bado upinzani unapinga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.