Pata taarifa kuu

Msumbiji: Zaidi ya watu 90 wamefariki katika ajali ya boti

Nairobi – Watu zaidia ya 90 wamepoteza maisha nchini Msumbiji, baada ya boti waliyokuwa wanasafiria kuzama hapo jana kwenye mkoa wa Nampula, wakielekea katika kisiwa kilichoko karibu na mji wa Lumbo.

Boti la wavuvi katika bahari ya Hindi, kaskazini mwa nchi ya Msumbiji.
Boti la wavuvi katika bahari ya Hindi, kaskazini mwa nchi ya Msumbiji. Getty Images - Eddie Gerald
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema huenda idadi hiyo ikaongezeka wakati huu maafisa wanapoendelea kuwatafuta abiria ambao huenda wamenusurika.

Wakati wa ajali hiyo, boti hiyo ilikuwa na abiria 130 wakiwemo watoto kadhaa.

Uchunguzi umeanzishwa ili kubaini kilichopelekea kuzama kwa boti hiyo lakini ripoti za awali, zinasema kuwa huenda, chanzo ni abiria kupita kiasi.

Maafisa wa serikali katika mkoa wa Nampula wanasema boti hiyo iligeuzwa kuwa Feri kuwasaidia watu kuvuka ngambo ya pili.

Aidha, imeelezwa kuwa watu hao walikuwa wanatoroka mkoa wa Nampula kwa hofu ya kupata maambukizi ya kipindupindu, ambapo visa 15,000 vimeripotiwa na vifo 32 tangu mwezi Oktoba mwaka uliopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.