Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

DRC: Watu 10 wauawa katika shambulio la wanamgambo wa CODECO katka kijiji cha Galayi

Watu kumi waliuawa katika shambulio la wanamgambo wa CODECO Jumamosi Aprili 6 katika kijiji cha Galayi, katika eneo la Banyali Kilo, huko Djugu katika mkoa wa Ituri, masharikimwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Gari la jeshi la Umoja wa Mataifa likipiga doria katika eneo la Djugu, mkoani Ituri, Machi 2018.
Gari la jeshi la Umoja wa Mataifa likipiga doria katika eneo la Djugu, mkoani Ituri, Machi 2018. ALEX MCBRIDE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na vyanzo vya ndani, wanawake wanne ni miongoni mwa wahanga.

Vyanzo hivyo vinaripoti kwamba ilikuwa karibu saa 11 Alfajiri kwa saa za ndani ndipo kundi la washambuliaji kutoka Andisa, Buraki, Wazabo na Dragi waliingia katika kijiji hiki kilicho kwenye kingo za Mto Ituri.

Walipofika, wanamgambo hao walifyatua risasi pande zote, na hivyo kusababisha mkanyagano kati ya watu waliokuwa na uoga.

Wanaume, wanawake na hata watoto, kwa kuchanganyikiwa kabisa, walijaribu kutoroka makazi yao na kukimbilia maeneo salama.

Wengine waliingia msituni na wengine kuelekea Mayalibo kijiji jirani.

Wanajeshi waliokuwa eneo jirani la eneo la tukio walijibu kwa risasi ili kuwafukuza wavamizi hao.

Ni katika mkanganyiko huu ambapo vyanzo kwenye tovuti vinataja idadi ya muda ya vifo bado ya angalau raia kumi, wakiwemo wanawake wanne.

Wanamgambo wawili pia waliuawa na askari mmoja wa FARDC aliuawa.

Idadi hii bado haijathibitishwa na vyanzo rasmi, kwa sababu msako wa kutafuta miili mingine unaendelea, hasa kuelekea kijiji cha Makalala ambako raia wengine wanasemekana kuuawa usiku huo huo na wavamizi hao.

Mauaji haya yanakuja siku moja baada ya mapigano kati ya CODECO na makundi ya waasi ya Zaire katika kijiji cha Rule huko Bahema Kaskazini.

Hii ilikuwa ni kulipiza kisasi mauaji ya raia mmoja na watu saba kutoka jamii ya Lendu walotekwa siku ya Jumatano katika kizuizi cha Iga na baadaye kuachiliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.