Pata taarifa kuu

Serikali ya DRC yakashifu matamshi ya Kadinali Ambongo kuhusu usalama

Nairobi – Serikali ya DRC, imeeleza kusikitishwa na matamshi iliyosema ya uchochezi aliyoyatoa Askofu Mkuu wa Kinshasa Kadinali Fridolin Ambongo wakati wa misa ya Pasaka mwishoni mwa juma lililopita, ambapo aliishutumu serikali kwa kuchangia kushuhudia kwa hali ya utovu wa usalama mashariki mwa nchi hiyo.

Askofu Mkuu wa Kinshasa Kadinali Fridolin Ambongo.
Askofu Mkuu wa Kinshasa Kadinali Fridolin Ambongo. AFP - ARSENE MPIANA
Matangazo ya kibiashara

Askofu Kadinali Fridolini Ambongo, wiki hii, aliwakashifu viongozi wakuu wa nchi hiyo kwa kushindwa kuwadhibiti waasi wa M23 wanaotatiza usalama mashariki mwa nchi hiyo, katika hotuba ya ujumbe wa sikukuu ya Pasaka kama alivyonukuliwa na mwanahabari wa idhaa ya Kifaransa, Pascal Mulegwa.

Katika hatua nyingine, kadinali Ambongo, aliwataka raia kuwa na umoja katika kukemea maovu na utovu wa usalama mashariki mwa nchi yao.

Patrick Muyaya ni waziri wa Habari na msemaji wa serikali ya DRC.

“Wakongomani wanaotaka kuchukua silaha kuwaua wenzao iliwapate madaraka wakati sisi tumechagua demokrasia, Inasikitisha.” alisema Patrick Muyaya ni waziri wa Habari na msemaji wa serikali ya DRC.

00:36

Patrick Muyaya

Raia wa Mashariki ya DRC wameendelea kukabiliwa na changamoto za kuisalama zinazotokana na makundi ya watu wenye silaha, mamia ya raia wakilazimika kuishi katika kambi za wakimbizi baada ya kutotoroka makazi yao.

Kinshasa inaituhumu jirani yake Kigali kwa kuendelea kuwaunga mkono waasi wa M23 wanaotekeleza mashambulio katika eneo la mashariki ya nchi, madai ambayo Kigali nayo imeendelea kukanusha.

Kwa sasa wanajeshi wa SADC wametumwa katika eneo hilo la nchi kusaidia katika vita dhidi ya makundi ya waasi, hatua inayokuja baada ya wanajeshi wa EAC kuondoka nchini DRC baada ya mamlaka ya Kongo kuwatuhumu kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.