Pata taarifa kuu
HAKI-UCHUNGUZI

Waziri Mkuu wa zamani wa Sudan Abdallah Hamdok alengwa na uchunguzi

Waendesha mashtaka wa Sudan, wanaoshirikiana na mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhane, walifungua uchunguzi siku ya Jumatano dhidi ya Waziri Mkuu wa zamani Abdallah Hamdok kwa tuhuma zinazoadhibiwa na hukumu ya kifo, televisheni ya taifa imesema.

Abdallah Hamdok alifutwa kazi wakati wa mapinduzi ya kijeshi yaliyoongozwa na Jenerali Burhane mwaka wa 2021.
Abdallah Hamdok alifutwa kazi wakati wa mapinduzi ya kijeshi yaliyoongozwa na Jenerali Burhane mwaka wa 2021. REUTERS - HANNIBAL HANSCHKE
Matangazo ya kibiashara

Β 

Bw. Hamdok, ambaye amekuwa akifanya mazungumzo kwa miezi kadhaa na waingiliaji kati wa Sudan na wa kikanda ili kumaliza vita vilivyoikumba nchi hiyo kwa takriban mwaka mzima, anatuhumiwa "kukiuka Katiba" na "kuchochea vita dhidi ya taifa", kulingana na televisheni ya serikali. Watu wengine kumi na watano, wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa na waandishi wa habari, wanalengwa na uchunguzi huu.

Abdallah Hamdok alifutwa kazi wakati wa mapinduzi ya kijeshi yaliyoongozwa na Jenerali Burhane mwaka wa 2021. Alichukua wadhifa huo mwaka wa 2019 kufuatia mapinduzi yaliyomwondoa Omar al-Bashir, baada ya miaka 30 madarakani. Sasa anaishi nje ya nchi, kama washtakiwa wengine.

Vita vya sasa, vilivyozuka Aprili 15, 2023 kati ya Jenerali Burhane na makamu wake wa zamani, Jenerali Mohamed Hamdane Daglo, mkuuwa Kikosi cha Wanajeshi wa Msaada wa Haraka (RSF), vimesababisha vifo vya maelfu ya watu na kusababisha zaidi ya watu milioni 8.5 kuyahama makazi yao , kulingana na Umoja wa Mataifa.

Kama sehemu ya juhudi zake za upatanishi, Waziri Mkuu wa zamani Hamdok alihitimisha makubaliano na Jenerali Daglo kuanza mazungumzo kwa nia ya kuondokana na mgogoro huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.