Pata taarifa kuu

Sudan: UN yaonya kuhusu uwezekano wa kutokea kwa baa la njaa

Nairobi – Sudan inahitaji hatua ya haraka, ili kukabiliana na baa la njaa ambalo limeendelea kusababisha magonjwa na maafa, kutokana na vita vinavyoendelea.

Maelfu ya raia wa Sudan wameripotiwa kutoroka makazi yao kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya pande mbili hasimu za kijeshi.
Maelfu ya raia wa Sudan wameripotiwa kutoroka makazi yao kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya pande mbili hasimu za kijeshi. REUTERS - ZOHRA BENSEMRA
Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya shirika la IPC, linalohusika na usalama wa chakula kwenye Umoja wa Mataifa, katika ripoti yake, imeonya kuwa hatua ya haraka inahitajika, kuwasaidia watu Milioni 5 wanaokabiliwa na baa la njaa.

Aidha, ripoti hiyo inapendekeza kusitishwa kwa vita mara moja kati ya jeshi na wanamgambo wa RSF ili kupelekwa kwa misaada ya binadamu kwa waathiriwa wa vita hasa walio kwenye jiji kuu Khartoum na majimbo ya Gezira, Darfur na Kordofan.

Hali hiyo inatarajiwa kuwa mbaya kati ya mwezi Aprili na Mei mwaka huu iwapo hatua za haraka hazitochukuliwa.

Onyo hili limekuja wiki hii tu baada ya Marekani kusema, itashinikiza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua hatua, ili misaada ya kibinadamu kama chakula na dawa, ziwafikie waathiriwa wa vita kupitia nchi jirani ya Chad, iwapo pande zinazopigana zitaendelea kuwa kikwazo kwa misaada hiyo kuwafikia walengwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.