Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Mchezaji wa soka wa Afrika Kusini auawa kwa kupigwa risasi Johannesburg

Beki wa kati wa klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini Luke Fleurs alipigwa risasi na kufa siku ya Jumatano wakati wa wizi mkali wa gari lake kwenye kituo cha mafuta, klabu yake na polisi wametangaza leo Alhamisi.

Luke Fleurs alishiriki katika Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2021 huko Tokyo, Japani.
Luke Fleurs alishiriki katika Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2021 huko Tokyo, Japani. © AP
Matangazo ya kibiashara

"Ni kwa huzuni kubwa tunatangaza kwamba mchezaji wa klabu ya Kaizer Chiefs, Luke Fleurs, alipoteza maisha yake jana usiku wakati wa jaribio la wizi wa gari lake huko Johannesburg," klabu hiyo ilichapisha kwenye mitandao ya kijamii.

Chiefs ni moja ya vilabu vikubwa zaidi vya kandanda nchini Afrika Kusini, mabingwa mara kumi na mbili wa Afrika Kusini, na waliofika fainali katika Ligi ya Mabingwa Afrika mnamo mwaka 2021. Fleurs ambaye alipata mafunzo na kufanya mazoezi ya kutosha huko Ubuntu Cape Town, mji alikozaliwa, kabla ya kuichezea SuperSport United kuanzia mwaka 2018 hadi 2mwaka 023, alishiriki katika Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2021 huko Tokyo. Pia aliitwa kwenye timu ya taifa lakini hakuwa na chaguo lolote.

Kulingana na polisi, kijana huyo mwenye umri wa miaka 24 alikuwa akisubiri kuhudumiwa kwenye gari lake la Gofu la Volkswagen wakati watu wawili waliokuwa wamejihami kwa bunduki walipofika kwenye gari na kuingia ndani. "Washukiwa walimtishia kwa bunduki na kumfanya ashuke kwenye gari, kabla ya kumpiga risasi sehemu ya juu ya mwili," amesema msemaji wa polisi, "mmoja wa washukiwa aliondoka na gari la mwathiriwa, akifuatiwa na msaidizi wake.

Mwanasoka huyo alitangazwa kufariki alipofikishwa hospitalini. Polisi wameanzisha uchunguzi na wanawasaka washukiwa hao, lakini hakuna aliyekamatwa kufikia Alhamisi asubuhi.

Uhalifu wa kikatili ni tatizo la mara kwa mara nchini Afrika Kusini, na ni suala la kisiasa tata katika maandalizi ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mnamo mwezi Mei. Nchi hii ilirekodi wastani wa karibu mauaji 84 kwa siku kati ya mwezi wa Oktoba na Desemba 2023, kulingana na takwimu rasmi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.