Pata taarifa kuu

Afrika Kusini: Spika wa Bunge akamatwa katika uchunguzi wa kashfa ya rushwa

Spika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula, amekamatwa Aprili 4, 2024, baada ya kwenda mwenyewe polisi, kama sehemu ya uchunguzi wa rushwa kuhusu kashfa hii tangu alipokuwa Waziri wa Ulinzi.

Nosiviwe Mapisa-Nqakula, wakati alipokuwa Waziri wa Ulinzi wa Afrika Kusini. (Picha hii ilipigwa mwaka 2012)
Nosiviwe Mapisa-Nqakula, wakati alipokuwa Waziri wa Ulinzi wa Afrika Kusini. (Picha hii ilipigwa mwaka 2012) Wikipédia
Matangazo ya kibiashara

"Atafikishwa mbele ya mahakama ya Pretoria" wakati wa mchana, Henry Mamothame, msemaji wa ofisi kuu ya mashtaka nchini Afrika Kusini, ameliambia shirika la habari la AFP, akithibitisha kukamatwa kwa Bi. Mapisa-Nqakula mapema asubuhi.

Siku ya Jumatano Aprili 3, Bi. Mapisa-Nqakula, alijiuzulu kwenye wadhifa wake husiana na tuhuma hizo, kilisema chama chake, cha ANC (kilichopo madarakani), miezi miwili kabla ya uchaguzi muhimu wa wabunge.

Spika wa Bunge tangu 2021 na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) yenye mamlaka yote ya ANC madarakani tangu kumalizika kwa utawala wa kibaguzi, Bi Mapisa-Nqakula, 67, anatuhumiwa kupokea kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa mwanakandarasi wa kijeshi alipokuwa Waziri wa Ulinzi (2014-2021).

Mahakama ilikataa rufaa ya dharura kutoka kwa spika wa Bunge siku ya Jumanne, na hivyo kuweka njia ya kukamatwa kwa mtu huyu wa chama tawala.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.