Pata taarifa kuu

Afrika Kusini: Spika wa Bunge, anayetuhumiwa kwa rushwa ajiuzulu

Rais wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula, anayelengwa na tuhuma za ufisadi, amejiuzulu, kimesema chama chake, ANC (kilichopo madarakani), Jumatano Aprili 3, miezi miwili kabla ya uchaguzi muhimu wa wabunge.

Nosiviwe Mapisa-Nqakula, Spika wa Bunge la Afrika Kusini, Desemba 13, 2022 wakati wa kikao cha Bunge mjini Cape Town.
Nosiviwe Mapisa-Nqakula, Spika wa Bunge la Afrika Kusini, Desemba 13, 2022 wakati wa kikao cha Bunge mjini Cape Town. AFP - GIANLUIGI GUERCIA
Matangazo ya kibiashara

"African National Congress (ANC) inaweza kuthibitisha kwamba barua ya kujiuzulu kutoka kwa Nosiviwe Mapisa-Nqakula imepokelewa rasmi," chama kimesema. ANC imethamini kujitolea kwake "kudumisha sura" ya chama kwa kuamua kung'atuka kabla hajaombwa kufanya hivyo, kimeongeza.

Spika wa Bunge tangu 2021 na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) yenye mamlaka yote ya ANC madarakani tangu kumalizika kwa utawala wa kibaguzi, Bi Mapisa-Nqakula, 67, anatuhumiwa kupokea kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa mwanakandarasi wa kijeshi alipokuwa Waziri wa Ulinzi (2014-2021).

Mahakama ilikataa rufaa ya dharura kutoka kwa spika wa Bunge siku ya Jumanne, na hivyo kuweka njia ya kukamatwa kwa mtu huyu wa chama tawala.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.