Pata taarifa kuu

Zaidi ya watu milioni 24 wanakabiliwa na njaa kusini mwa Afrika: Oxfam

Nairobi – Watu zaidi ya Milioni 24 wanakabiliwa na baa la njaa, utapiamlo na uhaba wa maji kwenye nchi za Kusini mwa Afrika kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa linaloshughulikia misaada ya binadamu la Oxfam.

Nembo ya shirika la Oxfam
Nembo ya shirika la Oxfam AFP - ANDY BUCHANAN
Matangazo ya kibiashara

Malawi yenye watu Milioni 19  imetajwa kuwa nchi iliyoathiriwa zaidi ambapo sehemu kubwa ya raia wake wanakabiliwa na changamoto hizo, zilizosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi hasa mafurko.

Nchini Zambia, watu Milioni Sita wameathiriwa huku wengine Milioni tatu nchini Zimbabwe na Msumbiji, wakikabiliwa na baa la njaa.

Oxfam kwenye ripoti yake imesema tangu mwezi Januari mwaka huu, mabadiliko ya tabia nchi kwenye ukanda wa nchi za Kusini mwa Afrika, hasa mafuriko, yamesbabaisha vifo vya zaidi ya watu 130 na kuharibu hekari Milioni 2 za mazao na kuharibu nyumba Elfu saba, pamoja na miundo mbinu nyingine kama barabara, vituo vya afya na mamia ya majengo ya Shule.

Shirika la Oxfam na washirika wake, wanahitaji Dola Milioni 15 ili kuwasaidia mamilioni ya watu waliothiriwa hasa na mafuriko baada ya kupoteza makaazi yao, kuwasaidia kupata maji safi ya kunywa na kuhakikisha kuwa haki za wanawake na wasichana zinaheshimiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.