Pata taarifa kuu

Senegal: Bassirou Diomaye Faye aapishwa na kuwa rais wa tano

Bassirou Diomaye Faye ameapishwa Jumanne Aprili 2, 2024 huko Diamniadio, na kuwa rais wa tano katika historia ya nchi hiyo. Anamrithi Macky Sall, mkuu wa nchi kutoka mwaka 2012 hadi 2024.

Wakati wa sherehe za kuapishwa kwa rais wa tano katika historia ya Senegal, Bassirou Diomaye Faye.
Wakati wa sherehe za kuapishwa kwa rais wa tano katika historia ya Senegal, Bassirou Diomaye Faye. © RTS
Matangazo ya kibiashara

 

Nchini Senegal, Bassirou Diomaye Faye, ambaye zaidi ya wiki mbili zilizopita alikuwa mgombea wa upinzani gerezani, mgombea urais badala ya Ousmane Sonko - kiongozi wa chama kilichofutwa cha African Patriots of Senegal PASTEF - na ambaye alichaguliwa kwa asilimia 54.3 katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais uliyofanyika Machi 24, 2024, kwa hivyo ameapishwa tu kama rais wa tano na mwenye umri mdogo zaidi katika historia ya nchi yake.

"Mbele ya Mungu na mbele ya Taifa la Senegali, ninaapa kutimiza kwa uaminifu majukumu ya rais wa Jamhuri ya Senegal, kuheshimu na kuzingatia kwa uangalifu masharti ya Katiba na sheria," amesema, akiinua mkono wa kulia mbele ya mamia ya maafisa wa Senegal na wakuu saba wa nchi za Afrika katika Kituo cha Maonyesho katika mji mpya wa Diamniadio, karibu na Dakar.

Taarifa zaidi zakujia,

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.