Pata taarifa kuu

Bassirou Diomaye Faye kutawazwa kuwa rais wa tano wa Senegal

Bassirou Diomaye Faye anatarajiwa kuapishwa leo Jumanne kuwa rais mteule wa Senegal, baada ya kushinda uchaguzi wa urais wa Jumapili iliyopita, ambapo atakabiliwa na changamoto si haba za kutatua kutokana na matarajio makubwa.

Wafuasi wa mgombea urais Bassirou Diomaye Faye wakikusanyika nje ya makao makuu ya kampeni baada ya matokeo ya awali kumtaja kuwa mshindi anayetarajiwa, huko Dakar, Senegal, Jumatatu, Machi 25, 2024.
Wafuasi wa mgombea urais Bassirou Diomaye Faye wakikusanyika nje ya makao makuu ya kampeni baada ya matokeo ya awali kumtaja kuwa mshindi anayetarajiwa, huko Dakar, Senegal, Jumatatu, Machi 25, 2024. AP - Mosa'ab Elshamy
Matangazo ya kibiashara

Rais mwenye umri mdogo zaidi wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, aliyechaguliwa kwa ahadi ya kuvunja mfumo uliowekwa, anaapishwa Jumanne Aprili 2 baada ya kupandishwa hadi kuwa rais na wananchi wa Senegal kwa asilimia 54.3.

Akiwa na umri wa miaka 44, Bassirou Diomaye Faye ni rais wa tano wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi tangu uhuru mwaka 1960.

Sherehe ya kuapishwa imepangwa kufanyika mapema asubuhi huko Diamniadio, karibu na Dakar. Bassirou Diomaye Faye anachukua mikoba ya Macky Sall, 62, ambaye aliongoza nchi yenye wakazi milioni 18 kwa miaka kumi na mbili na kudumisha uhusiano imara na nchi za Magharibi na Ufaransa. Viongozi kadhaa wa nchi, wakiwemo wawakilishi wa utawala wa kijeshi katika kanda ya Sahel, wanatarajiwa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwake.

Zoezi la kukabidhiana madarka kati ya rais anayemaliza muda wake Macky Sall na Rais Mteule Bassirou D. Faye litafanyika katika ikulu ya rais huko Dakar.

Zoezi hili la kukabidhiana madaraka, ambalo ni la tatu katika historia ya Senegal, unaashiria mwisho wa mvutano wa miaka mitatu kati ya Macky Sall na wawili walioshinda katika uchaguzi wa rais wa Machi 24: Bassirou D. Faye na yule ambaye, alikataliwa , kuwania uchaguzi Ousmane Sonko.

Akipongezwa na Paris, Washington na Umoja wa Afrika, uchaguzi wake uliosherehekewa na umati wa watu walioshangilia, ulitanguliwa na miaka mitatu ya mivutano na machafuko ambayo yalisababisha vifo vya makumi ya watu. Senegal, inayojulikana kama kisiwa cha utulivu katika Afrika Magharibi, ilipitia mgogoro mpya mwezi Februari wakati Rais Sall alipotangaza uamuzi wa kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais, na hivyo kuzidisha kutoaminiana kati ya sehemu ya wakazi na viongozi wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.