Pata taarifa kuu

Senegal: Bassirou Diomaye Faye kukabiliana na changamoto kubwa zinazoikumba nchi

Nchini Senegal, wakati rais mwenye umri mdogo zaidi katika historia ya nchi hiyo na bara la Afrika, Bassirou Diomaye Faye, 44, anatarajiwa kuapishwa leo, matarajio ya Wasenegal ni mengi. Akiwa amechaguliwa kwenye kiti cha urais kwa nia ya kutaka mabadiliko ya asilimia 54.3 ya wapiga kura waliomchagua katika duru ya kwanza, atakabiliwa na changamoto kubwa wakati wa kuapishwa kwake. Je, vipaumbele vyake vitakuwa vipi na atatumia mbinu gani kufikia malengo yake?

Bassirou Diomaye Faye anatarajia kuapishwa kuwa Rais mteule wa Senegal.
Bassirou Diomaye Faye anatarajia kuapishwa kuwa Rais mteule wa Senegal. AFP - JOHN WESSELS
Matangazo ya kibiashara

Muda tu baada ya kushinda uchaguzi, hotuba yake ya kwanza iligusia kupunguza gharama ya maisha, kupambana na ufisadi, kutafuta maridhiano ya kitaifa, ambapo siku ya Alhamisi alionesha ishara ya maridhiano kwa kukutana na rais anayeondoka Macky Sall.

Aidha Faye ameahidi kurejesha uhuru wa taifa hilo, kujadili upya mikataba ya mafuta na gesi, na kuboresha haki za uvuvi, lakini pia anaazimia kuondokana na matumizi ya faranga ya CFA, ambayo anaona ni urithi wa mkoloni wake Ufaransa.

Hata hivyo wachambuzi wa uchumi, wanaona kuwa kibarua kikubwa kwa Faye ni kubuniwa kwa nafasi za ajira, hali ambayo imewafanya vijana wengi kuwa miongoni mwa wahamiaji wanaojaribu kuvuka na kuingia Ulaya.

Mtihani mwingine ni kurejesha imani ya wapiga kura, ambapo Faye anatakiwa kuwapa uthibitisho wa mapema wa nia yake kwa kupunguza haraka bei ya bidhaa kama vile mchele, mafuta na umeme.

Faye pia atalazimika kuamua iwapo atalivunja Bunge lililochaguliwa Septemba 2022, ambalo chama chake hakina wabunge wengi.

Changamoto za kiuchumi

Akiwa ameifikishwa madarakani na wananchi wa Senegal kutaka mabadiliko, atalazimika kukabiliana na changamoto kubwa. Kupunguza gharama za maisha, kupambana na rushwa na kufanya kazi kuelekea usalama wa chakula ni baadhi ya miradi ya kipaumbele iliyoorodheshwa na Bassirou Diomaye Faye wakati wa taarifa yake ya kwanza kwa umma baada ya ushindi wake. Hatua kabambe ambazo zitahitaji rasilimali nyingi kutoka kwa Serikali. Katika mpango wake, Bassirou Diomaye Faye pia anaahidi kurejesha "uhuru" wa kiuchumi. Pamoja na mazungumzo ya mikataba ya mafuta na gesi, kwa mfano au mikataba ya uvuvi au hata kufanya kazi ya kuondokana na faranga ya CFA katika miaka ijayo na kuwekeza katika kilimo ili kufikia hatua ya kujitosheleza kwa chakula. Wakati wote akiwahakikishia wafadhili wa kimataifa kuhusu nia ya Senegal ya kubaki mshirika salama na anayetegemewa.

Lakini changamoto yake kuu, kulingana na wachambuzi kadhaa, itakuwa "kubuniwa kwa nafasi za ajira" katika nchi ambayo Wasenegal wawili kati ya watatu wako chini ya miaka 35 na ambapo kiwango cha ukosefu wa ajira kimefikia rasmi kwa 20%. "Kutatua tatizo la ukosefu wa ajira kutachukua muda na haitakuwa rahisi," anachanganua mwanauchumi Mame Mor Sene. Kwa sababu "ni muundo mzima wa uchumi ambao lazima urekebishwe". Kuwekeza katika sekta ya viwanda, kwa mfano, huku uchumi wa Senegal ukiegemea zaidi kwenye huduma.

Rais mpya atalazimika kukidhi matarajio yawananchi katika mazingira magumu ya kiuchumi. Mfumuko wa bei bado uko juu, ukuaji umepungua sana tangu janga la UVIKO-19 na vita nchini Ukraine. Senegal pia ni moja ya nchi zenye deni kubwa barani Afrika. Ikiwa na deni la karibu 75% ya Pato la Taifa, Senegal tayari ni nchi ya 12 yenye madeni zaidi barani na hivyo matumaini ya kupata deni kutoka kwa taasisi za kifedha ni madogo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.