Pata taarifa kuu

Senegal: Baraza la Katiba lamtangaza Faye kama rais aliyechaguliwa kwa 54.28% ya kura

Bassirou Diomaye Faye kwa kiasi kikubwa alishinda uchaguzi wa rais wa Senegal Machi 24 katika duru ya kwanza kwa 54.28% ya kura, mbele ya mgombea wa kambi tawala Amadou Ba (35.79%), kulingana na matokeo ya mwisho yaliyotangazwa siku ya Ijumaa na Baraza la Katiba.

Rais anayemaliza muda wake nchini Senegal Macky Sall (kulia) akikutana na Rais mteule wa Senegal Bassirou Diomaye Faye (kushoto) kwenye ikulu ya rais huko Dakar, Machi 28, 2024.
Rais anayemaliza muda wake nchini Senegal Macky Sall (kulia) akikutana na Rais mteule wa Senegal Bassirou Diomaye Faye (kushoto) kwenye ikulu ya rais huko Dakar, Machi 28, 2024. © AFP PHOTO / PRÉSIDENCE SÉNÉGALAISE
Matangazo ya kibiashara

Sasa imekuwa rasmi: Mwanasiasa wa upinzani nchini Senegal Bassirou Diomaye Faye ndiye rais wa tano wa Senegal. Akiwa na asilimia 54.28 ya kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi uliyofanyika Machi 24, anamzidi mshindi wa pili wa Macky Sall, Amadou Ba (35.79%), kulingana na matokeo ya mwisho yaliyotangazwa siku ya Ijumaa na Baraza la Katiba.

"Bwana Bassirou Diomaye Diakhar Faye amechaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Senegal", unabaini uamuzi wa Baraza la Katiba wa siku ya Ijumaa ambao shirika la habari la AFP lilipata kopi na kuthibitisha takwimu za muda zilizotangazwa Jumatano na mahakama.

Baraza "halijapokea upinzani wowote" kutoka kwa wagombea 19, wa tatu kati yao, Aliou Mamadou Dia, alipata 2.8% ya kura.

Bassirou Diomaye Faye ataapishwa siku ya Jumanne mchana katika mji mpya wa Diamniadio, ofisi ya rais imesema. Zoezi la kukabidhiana madaraka na mtangulizi wake Macky Sall linapangwa kufanyika katika ikulu ya rais huko Dakar.

Hii ni mara ya kwanza tangu Senegal ipate uhuru mwaka 1960 kwa mpinzani kushinda katika duru ya kwanza.

Ushiriki ulikuwa 61.30%. Hii ni chini ya mwaka wa 2019, wakati Rais anayemaliza muda wake Macky Sall alipata muhula wa pili, pia katika duru ya kwanza, lakini zaidi ya mwaka 2012.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.