Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Emmanuel Macron amwambia rais mteule wa Senegal kuhusu nia yake ya 'kuimarisha ushirikiano'

Emmanuel Macron ameeleza Ijumaa hii, Machi 29, 2024 kwa rais mteule wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, "nia yake ya kuendelea na kuimarisha ushirikiano kati ya Senegal na Ufaransa", wakati wa mazungumeo yao ya kwanza kwa njia ya simu tangu Bassirou Diomaye Faye kushinda uchaguzi wa Jumapili. 

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amezungumza na rais mteule wa Senegal Bassirou Diomaye Faye wakati wa mazungumeo yao ya kwanza kwa njia ya simu, "nia yake ya kuendelea na kuimarisha ushirikiano kati ya Senegal na Ufaransa.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amezungumza na rais mteule wa Senegal Bassirou Diomaye Faye wakati wa mazungumeo yao ya kwanza kwa njia ya simu, "nia yake ya kuendelea na kuimarisha ushirikiano kati ya Senegal na Ufaransa. MIGUEL MEDINA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa "amerejelea pongezi zake za dhati", zilizchapishwa siku ya Jumatatu jioni kwenye mitandao ya kijamii baada ya kutangazwa kwa ushindi wa Bassirou Diomaye Faye, na "kukaribisha jinsi uchaguzi huo ulifayika katika mazingira mazeuri na chaguo kuu la watu wa Senegal", imeripoti ikulu ya Élysée.

"Marais hao wawili hatimaye wamejadili sekta kuu ya ushirikiano wetu wa nchi mbili na hali ya kikanda," kulingana na vyanzo kutoka  upande wa Ufaransa.

Bassirou Diomaye Faye, mshindi katika duru ya kwanza ya uchagui, rais mteule wa Senegal, mwenye umri wa miaka 44, ataapishwa siku ya Jumanne. Akinufaika na msamaha wa rais, alitoka katika kifungo cha miezi 11 siku kumi kabla ya uchaguzi, wakati huo huo kama muelekezaji wake na kiongozi wa chama chao kilichofutwa cha PASTEF, Ousmane Sonko. Mpinzani wake mkuu, mgombea wa serikali Amadou Ba, mara moja alitambua kushindwa kwake.

Siku ya Jumatatu Bassirou Diomaye Faye alihakikisha kwamba nchi yake itasalia kuwa "mshirika salama na wa kutegemewa" wa washirika wote wa kigeni "wanaopewa heshima", wakati wa kuonekana kwake hadharani kwa mara ya kwanza tangu kutangazwa ushindi wake wa kihistoria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.