Pata taarifa kuu

Madagascar: Idadi ya waliofariki kutokana na kimbunga Gamane yaongezeka hadi 18

Idadi ya waliofariki kutokana na Kimbunga Gamane, kilichoikumba Madagascar ghafla siku ya Jumatano, imeongezeka hadi 18, huku nyumba zikisombwa na maji na zaidi ya watu 20,000 kulazimika kuyahama makazi yao, mamlaka imetangaza siku ya Ijumaa.

Barabara na madaraja mengi yamejaa maji kutokana na mafuriko. Baadhi ya watu walikufa maji, wengine waliuawa kwa kuporomokewa na nyumba au miti iliyoanguka, kulingana na mamlaka.
Barabara na madaraja mengi yamejaa maji kutokana na mafuriko. Baadhi ya watu walikufa maji, wengine waliuawa kwa kuporomokewa na nyumba au miti iliyoanguka, kulingana na mamlaka. © ELIE SERGIO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Upepo mkali uliangusha miti na mafuriko ya maji kukimbilia vijijini wakati kimbunga hicho kilipiga kisiwa cha Bahari ya Hindi mashariki mwa Afrika Kusini, lakini ambacho kilibadilisha mwelekeo na kupiga kaskazini siku ya Jumatano.

Kulingana na takwimu zilizochapishwa Ijumaa na Ofisi ya taifa ya Kudhibiti Hatari na Majanga (BNRGC), watu 18 wamefariki (ikilinganishwa na 11 katika ripoti ya awali), 20,737 walikimbia makazi na kaya 5,371 ziliathiriwa. Kwa sababu ya mafuriko, "hatuna chochote cha kula", na "watoto wetu wanaumwa kwa sababu ya maji machafu", Pasy, mkazi wa mkoa wa Sava, kaskazini-mashariki, ameliambia shirika la habari la AFP. 

"Tunaomba msaada," ameongeza, huku mvua ikinyesha, huku wakazi wakisaidiana kutoka kwenye kina kirefu cha maji na kwa wengine maji yakifika chini ya shingo zao, wakibeba vitu vya mwisho walivyoweza kuokoa. Barabara na madaraja mengi yamejaa maji. Baadhi ya watu walikufa maji, wengine waliuawa kwa kuporomokea na nyumba au miti iliyoanguka, kulingana na mamlaka.

"Hatuna cha kula. Akiba yetu yote ya makaa ya mawe imejaa maji na magunia ya mchele yamesombwa na maji. Hatujui la kufanya," amesema Fregin, mfanyabiashara wa eneo hilo. Kimbunga 

Gamane imeainishwa kama kimbunga cha kitropiki na kilitarajiwa kuondoka kisiwani Ijumaa alasiri, kulingana na wataalamu wa hali ya hewa. Msimu wa vimbunga kusini magharibi mwa Bahari ya Hindi kwa kawaida huchukua mwezi wa Novemba hadi mwezi wa Aprili, na hushuhudia karibu vimbunga kumi na mbili kwa mwaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.