Pata taarifa kuu

Uchaguzi wa urais Senegal: Amadou Ba ampigia simu Bassirou Diomaye Faye na 'kumpongeza'

Nchini Senegal, Amadou Ba, waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo na mgombea wa kambi tawala, amempigia simu "Bassirou Diomaye Faye kumpongeza na kumwombea", Jumatano Machi 25, 2024, amesema msemaji wa serikali, Abdou Karim Fofana, siku moja baada ya uchaguzi wa urais.

Mgombea wa muungano wa Rais Diomaye , Bassirou Diomaye Faye, akiashiria ushindi baada ya kupiga kura katika kituo cha École Ndiandiaye huko Ndiaganiao Machi 24, 2024 wakati wa uchaguzi wa urais wa Senegal.
Mgombea wa muungano wa Rais Diomaye , Bassirou Diomaye Faye, akiashiria ushindi baada ya kupiga kura katika kituo cha École Ndiandiaye huko Ndiaganiao Machi 24, 2024 wakati wa uchaguzi wa urais wa Senegal. AFP - SEYLLOU
Matangazo ya kibiashara

“Kwa kuzingatia mwelekeo wa matokeo ya uchaguzi wa urais na huku tukisubiri kutangazwa rasmi kwa mshindi, nampongeza rais Bassirou Diomaye Diakhar Faye kwa ushindi wake katika duru ya kwanza. " Ni katika taarifa fupi kwa vyombo vya habari kutoka kwa muungano wa Benno Bokk Yakaar ambapo Amadou Ba, mgombea wa kambi tawala katika uchaguzi wa Machi 24, 2024, amekiri kushindwa dhidi ya mpinzani wa chama kilichofutwa cha PASTEF .

Katika taarifa hii, Waziri Mkuu wa zamani anatangaza "kumtakia mafanikio mengi na ujasiri kwa ustawi wa raia wa Senegal".

Msemaji wa serikali Abdou Karim Fofana amebaini kwa upande wake kwamba Amadou Ba amemwita mpinzani wake "kumpongeza".

Matokeo ya muda ya uchaguzi huu yatatangazwa kabla ya Jumanne jioni katika ngazi ya idara, kisha kutangazwa kabla ya Ijumaa Machi 19 na Mahakama ya Rufaa ya Dakar, katika ngazi ya kitaifa.

Mnamo Machi 24, Wasenegal milioni 7.3 waliitwa kupiga kura kumchagua mkuu wa tano wa nchi, baada ya Léopold Sédar Senghor (1960-1980), Abdou Diouf (1981-2000), Abdoulaye Wade (2000-2012) na Macky Sall (2012) -2024).

Awali uchaguzi uliokuwa ulipangwa kufanyika Februari 25, ambao kuahirishwa kwake kuliiingiza nchi katika mzozo mkubwa wa kisiasa.

Endelea kufuatilia taarifa zetu kupitia sw.rfi.fr

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.