Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-DEMOKRASIA

Senegal inafanya uchaguzi wa urais, uliosubiriwa kwa muda mrefu

Nchini Senegal, watu milioni 7.3 wanatarajiwa kupiga kura Machi 24, 2024, kuamua kati ya wagombea 17 ambao bado wako kwenye kinyang'anyiro cha kumrithi Macky Sall, ambaye ameongoza nchi hiyo tangu mwaka 2012. Hapo awali uchaguzi huu wa urais uliopangwa Februari 25, uliahirishwa kufuatia mzozo mkubwa wa kisiasa.

Uchaguzi wa urais nchini Senegal unafanyika Machi 24, 2024. Fuata matangazo yote ya RFI-KSWAHILI kwenye sw.rfi.fr.
Uchaguzi wa urais nchini Senegal unafanyika Machi 24, 2024. Fuata matangazo yote ya RFI-KSWAHILI kwenye sw.rfi.fr. © Studio graphique FMM
Matangazo ya kibiashara

Unachotakiwa kuelewa

► Nchini Senegal, nchi yenye wakazi milioni 18, karibu milioni 7.3 wanatarajiwa kushiriki katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2024, Jumapili hii, kati ya saa 8 asubuhi na saa 12 jioni, saa za ulimwengu na za ndani. Kura ya kumchagua rais wa tano wa Senegal, baada ya Léopold Sédar Senghor (1960-1980), Abdou Diouf (1981-2000), Abdoulaye Wade (2000-2012) na Macky Sall (2012-2024).

► Kuna wagombea 17 ambao wanaenelea kushiriki kinyang'anyiro hiki cha urais kumrithi Macky Sall: Amadou Ba, Boubacar Camara, Aliou Mamadou Dia, Mamadou Lamine Diallo, El Hadji Mamadou Diao, Mahammed Boun Abdallah Dionne, Déthié Fall, Papa Djibril Fall, Bassirou Diomaye Faye, El Hadji Malick Gakou, Serigne Mboup, Daouda Ndiaye, Aly Ngouille Ndiaye, Anta Babacar Ngom, Khalifa Sall, Thierno Alassane Sall, Idrissa Seck.

► Vituo 16,440 vya kupigia kura vinatarajiwa kufunguliwa Machi 24, pamoja na 807 nje ya nchi. Matokeo ya muda ya duru hii ya kwanza yatatangazwa kabla ya Ijumaa Machi 29. Katika tukio la duru ya pili, hii itaandaliwa Jumapili ya pili baada ya Baraza la Katiba kutangaza matokeo ya mwisho ya duru ya kwanza.

► Muhula wa Macky Sall unamalizika tarehe 2 Aprili. Mnamo Februari 3, mkuu wa nchi anayemaliza muda wake alitangaza kuahirishwa kwa uchaguzi huu uliopangwa kufanyika Februari 25. Bunge lilipanga kufanyika uchaguzi tarehe 15 Desemba. Tarehe iliyokataliwa na Baraza la Katiba. Mwishoni mwa mdahalo wa kitaifa uliosusiwa na wagombea urais wengi, Juni 2 ilipendekezwa. Tarehe ambayo pia ilifutiliwa mbali na Baraza la Katiba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.