Pata taarifa kuu

Faida haramu kutokana na kazi za kulazimishwa duniani imefikia Dolla Bilioni 236

Nairobi – Faida haramu kutokana na kazi za kulazimishwa duniani kote imeongezeka hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 236 kwa mwaka, limeripoti shirika la kazi duniani ILO.

Nembo ya shirika la kazi duniani ILO.
Nembo ya shirika la kazi duniani ILO. ILO
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa ILO, karibu robô tatu ya mapato haramu yaliyopatikana, yanatokana na dhulma za kijinsia, hali inayowafanya wahalifu walioko nyuma ya biashara ya ngono kukwepa kodi.

Wataalamu wa shirika hilo wanasema kumekuwa na ongezeko la asilimia 37 ikilinganishwa na makadirio ya mwisho yaliyochapishwa muongo mmoja uliopita, hii ikiwa ni idade kuwa zaidi ya watu kunyanyaswa kutokana na kazi wanazofanya.

Takriban watu milioni 6 na laki 3 walikabiliwa na dhulma za biashara ya ngono katika miaka mitatu iliyopita , huku watu wanne kati ya watano walioathirika walikuwa wasichana au wanawake, watoto wakichangia zaidi ya robo ya kesi zote, ilisema ripoti ya ILO.

Kazi za kulazimishwa katika tasnia ya viwanda ilifikia dola bilioni 35, ikifuatiwa na watoa huduma iliyokuwa dola bilioni 21, kilimo dola bilioni 5 na kazi za nyumbani dola bilioni 2 na laki 6, alisema kiongozi wa jopo lililofanya utafiti huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.