Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

CAR: Miezi 3 baada ya kukamatwa kwa mbunge wa upinzani, familia yake yaomba aachiliwe huru

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, mbunge wa upinzani Dominique Yandocka anashikiliwa kwa muda wa miezi mitatu. Alikamatwa mnamo Desemba 15 na kuwekwa kizuizini, licha ya kinga yake ya ubunge, Dominique Yandocka anatuhumiwa kwa "njama na jaribio la mapinduzi ya kijeshi", baada ya kukamatwa na "kupatikana na hatia", kulingana na mwendesha mashtaka. Mawakili wake na familia yake wanaendelea kuomba aachiliwe huru, wakati utaratibu hausongi mbele.

Afisa wa polisi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati akishika doria katika mojawapo ya ofisi za manispaa za wilaya nane za Bangui, hapa ilikuwa mwaka wa 2015 (picha yakielelezo).
Afisa wa polisi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati akishika doria katika mojawapo ya ofisi za manispaa za wilaya nane za Bangui, hapa ilikuwa mwaka wa 2015 (picha yakielelezo). RFI/Laurent Correau
Matangazo ya kibiashara

Ombi lao la kuachiliwa rasmi halikujibiwa, mawakili wa Dominique Yandocka walituma ukumbusho kwa mkuu wa majaji wa uchunguzi. Wanaendeleza hoja zile zile: kulingana na wao, upande wa mashtaka haujawahi kuthibitisha "madai" uliotoa ili kuhalalisha kuzuiliwa kwa mbunge, ambaye ana kinga yake ya ubunge.

Wanaomba hasa apewe nafasi ya kuhudumiwa kimatibabu, kwa sababu mbunge huyo ana matatizo ya moyo na figo yanayosababishwa na kuwekwa kizuizini, anaeleza binti yake, Ashley Yandocka: "Ninaomba ushahidi kama wa kutosha unaoeleweka na zaidi ya yote msaada katika suala la huduma ya afya, kwa sababu baba yangu kwa sasa ni mgonjwa sana, kutokana na shinikizo alilonalo. Kwa hiyo, naomba tuliangazie jambo hili na kumwachilia Dominique Yandocka na kupewa matibabu. "

Wakili Bruno Gbiegba, mmoja wa wanasheria wake, aliweza kumtembelea wiki hii na kumshawishi kusitisha mgomo wa kula aliouanzisha siku chache zilizopita. Ujumbe kutoka afisi ya Bunge pia ulienda kumuona katika kambi ya Roux. Akihojiwa siku ya Jumatatu na vyombo vya habari vya serikali, msemaji wa serikali alikataa kutoa maoni yake kuhusu "hatua zinazoendelea za kisheria". "Tunapaswa kwenda hadi mwisho kujua ukweli," alisema Maxime Balalou.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.