Pata taarifa kuu
HAKI-SIASA

CAR: Kiongozi wa upinzani aachiliwa kwa muda kabla ya kesi

Mahakama mjini Bangui siku ya Jumatano ilimegiza kuachiliwa kwa muda kwa mmoja wa wapinzani wakuu knchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Crépin Mboli Goumba, na kuahirisha kesi yake ya "kuchafua" na "kudharau mahakama" hadi Machi 13, kulingana na mwandishi kutoka shirika la habari la AFP, aliye hudhuria kikao hicho.

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Faustin-Archange Touadera, kwenye Mkutano Mkuu wa 78 wa Umoja wa Mataifa, Septemba 21, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Faustin-Archange Touadera, kwenye Mkutano Mkuu wa 78 wa Umoja wa Mataifa, Septemba 21, 2023. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Mashirika yasiyo ya kiserikali ya kimataifa ya haki za binadamu mara kwa mara yanashutumu ukandamizaji wa upinzani wote katika taifa hili la Afrika ya Kati, linaloainishwa na Umoja wa Mataifa kama mojawapo ya nchi nne zenye maendeleo duni zaidi duniani.

Baada ya siku tatu chini ya ulinzi wa polisi, Wakili Mboli Goumba, mratibu wa jukwaa kuu la upinzani dhidi ya mamlaka ya Rais Faustin Archange Touadéra, alifika mbele ya chumba cha mahakama kuu katika mji mkuu Bangui.

"Baada ya ombi la kufutwa kazi kutoka kwa mawakili wake", mshtakiwa "ameachiliwa kwa muda kwa marufuku ya kuondoka Bangui", amesema jaji Matthieu Nana Bibi ambaye ameongoza kesi hiyo.

"Nimejitayarisha kiakili kustahimili kila kitu kitakachofuata katika kesi hii, kwa kulaani kutofanya kazi kwa mfumo wa haki wa Afrika ya Kati," Bw. Mboli Goumba ameiambia hadhira.

Ni wazi kuwa amedhoofika kidogo lakini akiwa na tabasamu usoni, ameondoka na polisi kusaini ripoti yake ya kuachiliwa kwake katika majengo ya mahakama, huku wafuasi wachache wakipiga kelele "ameachiliwa, ameachiliwa!". Kulingana na chama chake, wakili Mboli Goumba pia ana uraia wa Marekani.

Kiongozi wa Chama cha African Party for Radical Transformation and Integration of States (PATRIE) na mratibu wa Kambi ya Jamhuri ya Kutetea Katiba (BRDC), jukwaa muhimu zaidi la upinzani, alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Bangui siku ya Jumapili akiwa ndani ya ndege iliyokuwa karibu kupaa kuelekea Cameroon.

Upande wa mashtaka ulitangaza siku ya Jumatatu kwamba alifunguliwa mashtaka haswa kwa maoni yaliyotolewa mnamo Februari 20 wakati wa mkutano wa waandishi wa habari wa PATRIE na "uwezekano wa kusema kama kashfa na kudharau mahakama".

Utawala ulioshutumiwa na Human Rights Watch

Siku hiyo, wakili Mboli Goumba aliwashutumu baadhi ya majaji kwa kuridhika na washtakiwa au hata kuwa wafisadi, maneno ambayo aliyarudia siku iliyofuata katika mahojiano na Radio France Internationale (RFI) akikemea "haki isitendeke tena kwa niaba ya raia.”

Upinzani, ambao mikutano na maandamano yao yanakaribia kupigwa marufuku kimfumo, pia mara kwa mara yanakabiliwa na vitisho , mashirika yasiyo ya kiserikali ya kimataifa yanashutumu mara kwa mara.

Mbunge wa upinzani, Dominique Yandocka, amefungwa tangu Desemba 15, licha ya kinga yake ya ubunge, kwa "jaribio la mapinduzi" ambayo upande wa mashtaka bado haujathibitisha hadharani.

Utawala wa Bw. Touadéra "unakandamiza mashirika ya kiraia, vyombo vya habari na vyama vya siasa vya upinzani", liliandika shirika la Human Rights Watch (HRW) mwezi Aprili 2023, likitaja "wasiwasi mkubwa kuhusu hatari katika suala la ukiukwaji wa haki za binadamu na kupunguzwa kwa nafasi ya kidemokrasia na uhuru wa kujieleza.

Shirika hili pia limeitaka serikali ya Bw. Touadéra "kuhakikisha uhuru wa mahakama ili kuhakikisha kwamba wale waliohusika wanaoshambulia wakosoaji wa serikali wanachukuliwa hatua."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.