Pata taarifa kuu

CAR: Mlinda amani wa Cameroon auawa baada ya kukanyaga bomu la kutegwa ardhini

Mlinda amani wa Cameroon aliuawa Jumatatu na wengine watano kujeruhiwa na mlipuko wa bomu la kutegwa ardhini, kaskazini-magharibi mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati ambapo makundi ya waasi yanapambana mara kwa mara na jeshi na washirika wake mamluki wa Urusi kutoka kundi la Wagner, Umoja wa Mataifa umetangaza.

Mlinda amani wa Minusca anashika doria katika wilaya ya PK12 ya Bangui ambako wapiganaji wa CPC waliendesha mapigano mnamo Januari 13.
Mlinda amani wa Minusca anashika doria katika wilaya ya PK12 ya Bangui ambako wapiganaji wa CPC waliendesha mapigano mnamo Januari 13. AFP - FLORENT VERGNES
Matangazo ya kibiashara

 

Wanajeshi kutoka kikosi cha Cameroon cha ujumbe wa kulinda amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA, walikuwa wakisindikiza timu ya Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) wakati bomu hilo lilipolipuka wakati msafara huo ukipita katika kijiji cha Mbindale, takriban kilomita 450 kaskazini mwa Bangui, inabainisha MINUSCA katika taarifa ambayo shirika la habari la AFP limepata kopi siku ya Jumatano.

Wawili kati ya waliojeruhiwa walijeruhiwa "vibaya" na wote walipelekwa hadi hospitalini, kulingana na MINUSCA. Mlipuko huu ulitokea takriban kilomita ishirini kutoka mahali ambapo waasi kutoka kundi la  3R (Reclamation and Rehabilitation) waliwauwa raia 23 mnamo Desemba 21, katika kijiji cha Nzakoundou, ambapo kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kilitumwa.

3Rs ni mojawapo ya makundi yenye silaha yenye nguvu zaidi kati ya makundi mengi ya waasi au magenge ya wahalifu yanayoendesha ukatili wao katika eneo hilo. Makundi haya, lakini pia jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati na washirika wao wa Urusi, mara kwa mara wanashutumiwa na mashirika yasiyo ya kiserikali ya kimataifa na Umoja wa Mataifa kwa uhalifu na dhuluma dhidi ya raia.

Mwezi wa Julai mwaka uliyopita, askari wa kulinda amani wa Rwanda aliuawa wakati wa shambulio lililotekelezwa na kundi lisilojulikana lililokuwa na silaha dhidi ya doria ya Umoja wa Mataifa mashariki mwa nchi hiyo. Tangu mwaka 2022, wanajeshi watano wa MINUSCA waliuawa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, kulingana na takwimu za umoja huo.

Moja ya nchi maskini zaidi duniani, Jamhuri ya Afrika ya Kati imekuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu mwaka 2013, wakati muungano wa makundi yenye wapiganaji wengi wa Kiislamu, Séleka, ulipompindua Rais François Bozizé. Kisha Bozizé alipanga na kuwapa silaha wale walioitwa wanamgambo wa anti-balaka, hasa Wakristo na waaminifu, ili kujaribu kupata tena mamlaka.

Mapigano kati ya makundi haya, ambayo raia walikuwa waathiriwa wakubwa, yalifikia kilele mnamo 2018 kabla ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, hadi wakati huo mbaya sana, vilipungua kwa kasi, na kubadilika kuwa vita vya msituni vilivyoongozwa na waasi au makundi ya uporaji wa rasilimali za nchi, hasa dhahabu na almasi.

3R, kundi la zamani la waasi wa Sélekas, walijiunga na uasi wa Muungano wa Wazalendo wa Mabadiliko (CPC) ambao ulianzisha mashambulizi makubwa dhidi ya Bangui mnamo Desemba 2020 kujaribu kupindua mamlaka ya Rais Faustin Archange Touadera.

Touadera alitoa wito kwa Moscow kuokoa jeshi maskini na lenye mafunzo duni na mamia ya wanamgambo wa Urusi walikuja kuimarisha ulinzi na kujiunga na mamia ya wengine ambayo tayari yalikuwepo tangu 2018, kusaidia kuwaondoa waasi kutoka kwa maeneo mengi waliyokuwa wakishikilia. Hata hivyo, mamlaka ya serikali kuu haijaanzishwa tena katika baadhi ya maeneo ya mbali ya nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.